Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMII YATAKIWA KUWALINDA WENYE ULEMAVU

Katibu wa Kambi mtaa wa mkolani 2022 wa kanisa la waadventista wasabato akizungumza kwenye uzinduzi wa sikuu za vibanda ambazo hufanyika kwa mwaka mara moja, Janeth Tongora.

***********************

Na SHEILA KATIKULA, MWANZA

Jamii imetakiwa kuwathamini,kuwalinda na kuwapenda watu wenye ulemavu kwa kuwatendea mema na siyo kuwafanyia vitendo vya ukatili.

Hayo yamesemwa jana na Katibu wa Kambi mtaa wa mkolani 2022 wa kanisa la seventhday waadvestinta wasabato ,Janeth Tongora wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa sikuu za vibanda ambazo hufanyika kwa mwaka mara moja iliyowakutanisha washilika kutoka kwenye makanisa mbalimbali yakiwemo Mkolani,Nyahingi Hili,Nyamazobe na Agape.

Amesema sikuu za vibanda hufanyika kwa mwaka mara moja ambapo hushikila washilika kutoka kwenye makanisa mbalimbali kwa lengo la kumcha mungu kwa pamoja.

Amesema ni wajibu wa kila mtu kuona umuhimu wa kuwalinda na kuwathamini watu wenye ulemavu kwa sababu ni zawadi kutoka kwa mungu.

Amesema ni kosa kumfungia ndani mtu wenye ulemavu kwa sababu ya anahaki ya kufanya kazi na kuishi bila kufanyiwa vitendo vya ukatili.

"Inaskitisha kuona baadhi ya watu huwafungia ndani watoto wao wenye ulemavu kwani kufanya hivyo ni kosa na hupelekea kumnyima haki zake za msingi ikiwamo elimu.

"Tutakaa hapa kwa siku saba tukiwa na lengo la kuomba kwa pamoja na kukumbushana jinsi ya kulea watoto katika maadili mema,kupiga ukatili, jinsi ya kuishi kwenye ndoa kwa amanii na upendo,"amesema Tongora.

Naye Witness Bukumbi ambaye ni mshilika wa kutoka kwenye kanisa la Mkolani amesema Siku hizo za vibanda hufundisha mambo mbalimbali ikiwamo kuishi na vizuri na jamii,kulea Eaton katika maadili mema na kukumbushana kufanya kazi kwa bidii.

Amewaomba washilika kuzingatia mafundisho yanatolewa na viongozi wao wa dini ili wawaze kuyafanyika kazi.

Post a Comment

0 Comments