Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT.PAULINA-VIJANA WAPO TAYARI KUJITOKEZA KUHESABIWA

Mbunge Viti Maalum Kundi la Vyuo Vikuu Dkt.Paulina Nahato akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Temeke pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa uliofanyika leo Agosti 19,2022 Temeke Jijini Dar es Salaam. Mbunge Viti Maalum Kundi la Vyuo Vikuu Dkt.Paulina Nahato akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Temeke pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa uliofanyika leo Agosti 19,2022 Temeke Jijini Dar es Salaam.

******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mbunge Viti Maalum Kundi la Vyuo Vikuu Dkt.Paulina Nahato amesema vijana Vyuo Vikuu wanatambua umuhimu wa kuchangia maendeleo ya taifa kwa ujumla hivyo ni wajibu wa kila kijana kushirikia kikamilifu kufanikisha zoezi la sensa linalotarajia kufanyika Agosti 23,2022.

Ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Temeke pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa uliofanyika leo Agosti 19,2022 Temeke Jijini Dar es Salaam.

Amesema vijana na watanzania kwa ujumla wanaitajika kujitokeza kuunga jitihada za serikali ili kuweza kutambua idadi ya wananchi wake ili iwe rahisi kuweza kupanga maendeleo.

"Rais Samia Suluhu Hassan pamoja ana malengo mazuri kwa watanzania hivyo hakuna budi kwa umoja wetu kushiriki katika zoezi hili la sensa kwani ni njia mojawapo kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake". Amesema Dkt.Paulina.

Post a Comment

0 Comments