Ticker

6/recent/ticker-posts

NSSF IMEFANIKIWA KUKUSANYA 1.42 KWA MWAKA 2021/2022

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa NSSF Masha Mshomba

********************

Na Magrethy Katengu

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),katika kipindi cha mwaka 2021/2022 umepata mafanikio makubwa ikiwemo kukusanya makusanyo michango tilioni 1.42 na kuandikisha wanachama wapya huku wastaafu wakilipwa na stahiki zao huku wakitatua baadhi ya walio na malalamiko juu ya Mfuko huo.

Akizungumza na Waandishi habari leo Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa NSSF Masha Mshomba amesema wakati akitoa taarifa ya Utendaji wa Mfuko pamoja na Vipaumbele vya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambapo Mfuko huo inatarajia kusajili wanachama wapya laki tatu thelathini na tatu mianne sabini na nane sawa ongezeko la asilimia 34 .

"Tumepata mafanikio makubwa katika suala zima ukusanyaji wa makusanyo ambayo yalizidi bajeti tuliopangiwa na serikali hii imetokana na Mfumo wa kielekroniki hiyo ni chachu ya ukuaji wa Mfuko na hivyo ukusanyaji huo umesababishwa na sababu kadhaa ikiwemo kuweka misingi imara na madhubuti ya ukusanyaji wa mapato," alisema.

Mshomba alisema ukuaji huo ni mkubwa tofauti na miaka miwili ya nyuma iliyopita ambapo thamani ya Mfuko ilikuwa ni Shilingi Trilioni 4.3 na kuwa ukuaji huo umechangiwa na ongezeko la makusanyo ya michango.

Hata hivyo amesema katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022, Mfuko ulikusanya zaidi ya Shilingi Trilioni 1.42 kwamba makusanyo hayo ni zaidi ya hata bajeti ambayo waliojipangia iliyokuwa Shilingi Trilioni 1.38 hivyo wakavuka lengo

Mshomba amesema pia Mfuko umeboreshaji sana udhibiti wa matumizi jambo na mbalo limechangia ukuaji wa NSSF.

Mafanikio mengine yaliyopatikana, alisema ni uboreshaji wa huduma hasa kwa kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA ambapo sasa mwanachama na wadau wanaweza kupata huduma popote walipo bila ya kufika katika ofisi za NSSF kwa kutumia mifumo ya waajiri na wanachama yaani Employer Potal na Member Potal.

Mshomba amesema Mfuko pia unapata matokeo mazuri sana katika Uwekezaji hasa ukizingatia kuwa wanawekeza katika maeneo salama ambapo katika kipindi cha miaka miwili uwekezaji umeleta mapato makubwa.

"Ilikuwa haijafikiwa NSSF kuweza kupata mapato ya mwaka zaidi ya Shilingi bilioni 500 lakini katika mwaka huu wa fedha umepata zaidi ya Shilingi bilioni 600," alisema.

Amesema matokeo hayo ya uwekezaji yametokana na Mfuko kujikita zaidi katika uwekezaji kwenye maeneo ambayo yanaleta faida kwa Mfuko na kuhakikisha wanaongeza wanachama wapya.

Mshomba amesema chachu kubwa ya mafanikio ya NSSF imechagizwa na kasi ya utendaji wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu amekuwa chachu ya ongezeko kubwa la wawekezaji hapa nchini.

Aidha Mshomba amewahamasisha Watanzania wote kushiriki katika zoezi zima la Sensa ya Watu na Makazi ifikapo tarehe 23 Agosti, 2022 ili waweze kuhesabiwa.

Post a Comment

0 Comments