Ticker

6/recent/ticker-posts

GURUDEV AMALIZA “ROYAL TOUR”NA SALAAM KWA WASANII

Kiongozi mashuhuri duniani wa kiroho na Balozi wa Amani, Gurudev Sri Sri Ravishankar ameondoka nchini leo asubuhi kuelekea Ujerumani baada ya kukamilisha “Royal Tour” ya siku mbili nchini.

Akiwa hapa nchini,pamoja na mambo mengine, alihudhuria Tamasha la Utamaduni la Tanzania na India, kuendesha mazoezi ya kutumia njia za kupumua, kuhutubia mkutano wa Biashara kati ya Tanzania na India na kutembelea Zanzibar ambako pia alikutana na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi.

Akiagana kwenye hotel ya Hyatt na baadaye Uwanja wa Ndege na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, Bw. Gurudev ameahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika sekta za utamaduni na michezo ikiwemo kuahidi kualika vikundi vya sanaa na utamaduni kuhudhuria Tamasha lake kubwa liitwalo “World Cultural Festival” ambalo mwaka jana lilihudhuriwa na wasanii 37,000 kutoka nchi 155 duniani na likikusanya takribani watu milioni 3.7 pamoja.


Post a Comment

0 Comments