Ticker

6/recent/ticker-posts

MENEJA RUWASA TANGA ATEMBELEA MIRADI YA MAJI PANGANI, ATOA MAAGIZO KUHUSU WASIOJIWEZA.

Meneja Lugongo akiongozwa na Diwani Kimweri kupanda juu kukagua mradi wa Tanki la maji.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga Upendo Lugongo akitoa maelekezo kwa msimamizi wa ujenzi wa mradi wa Tanki la maji katika kata ya Mkalamo, Mhandisi Shija Yunza.
Diwani wa kata ya Mkalamo Adam Kimweri akitoa maelezo kwa Meneja Lugongo wakiwa katika ujenzi wa mradi wa tanki Sakura kata ya Kwakibuyu.
Meneja Lugongo akikagua mchanga unatumika kujengwa mradi wa Maji unaoendelea katika kijiji cha Sakura, kata ya Kwakibuyu.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga Upendo Lugongo akikagua ujenzi wa mradi wa kisima.
Meneja Lugongo akiwa na timu yake ya Wilaya ya Pangani katika kituo cha blonde la mto Pangani.


********************

Na Hamida Kamchalla, PANGANI.


MENEJA wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Tanga, Upendo Lugongo amesema wananchi wanaotumia maji yanayosambazwa na RUWASA wanapaswa kulipia kama wanavyolipia huduma zingine muhimu za kijamii ili miradi hiyo iweze kujiendesha.


Lugongo ameyasema hayo alipotembelea miradi ya maji katika Wilaya ya Pangani akiwa katika mradi wa kata ya Mkalamo ambapo alisisitiza viongozi husika kusimamia ipasavyo ili kuhakikisha wananchi wakipata maji walipie kiasi cha sh elfu moja kwa mwezi.


Amesema visima vyote hata vile vya bomba la kubembea ikiwezekana vifungwe ili wananchi watambue juhudi za serikali na waweze kuchangia huduma hiyo.


"Mbona mtu anaweza kuiweka vocha kwenye simu ya sh elfu moja kwa siku halafu ashindwe kulipia sh elfu hiyo kwa mwezi, siyo kweli, kwahiyo ni lazima hicho kitu kikasimamiwe",


"Mwenyekiti nikuombe, tuimarishe ushirikiano watu hata kama wanatumia visima vya bomba la kubembea, walipie kwasababu mali yote ni ya umma na serikali, na serikali ndiyo hawa wananchi, suala la kulipia siyo la kujadiliana" amesema Lugongo.


Aidha amebainisha kwamba sheria ilishaelekeza kwamba kwa wale ambao hawana uwezo wasilipie huku akiwataka viongozi wakiwemo madiwani na Wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanawatengea huduma hiyo bila malipo.


"Waheshimiwa madiwani na Wenyeviti mnawafahamu vizuri wananchi wenu ambao hawana uwezo, basi muanue kuwatengea kila mtu kama ni ndogo zake 10 kila siku, kwasababu jamii zetu zinatofautiana, kwahiyo muainishe na ninyi ili wale nao wapate maji ya uhakika" amesma.


"Lakini pia kuna nyumba za mayatima, kama zipo nao kawapeni maji, watu wengine watafidia zile bili za majibyanayoenda kwenye zile nyumba" amesisitiza Lugongo.


Amefafanua kwamba kwenye nyumba za ibada na mashuleni kwakuwa wana uwezo wa kulipia kama wanavyoendesha shuhuli mbalimbali wanpokuwa katika maeneo yao.


"Lakini nyumba za ibada zote ni lazima zilipie kwasababu Kuna waumini kule wana uwezo, shule ni lazima walipie kwasababu kuna watoto wenu pale, kama mnaweza kuwapa chakula na maji nyumbani kwanini mshindwe kulipia Hilo shuleni, hilo pia haliwezekani" amebainisha.


Naye Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Pangani, Wilbroad Mngereza amesema miradi katika Wilaya hiyo kuna jumla ya miradi 15 inayotekelezwa na RUWASA ambapo miradi mitano ya matanki ya maji iliyotembelewa mitatu imetokana na fedha za Uviko 19 na miwili ni fedha za force account.


"Miradi mitano ya matanki ya maji umegarimu kiasi cha zaidi ya sh bilioni 2,835, mradi kata ya Mkalamo umegarimu zaidi ya sh milioni 507, kata ya Mikinguni sh milioni 534, kata ya Kwakibuyu sh milioni 594, kata ya Mwera (Ushongo) sh milioni 500 na kijiji cha Meka kata ya Ubangaa umegarimu sh milioni 700" amesema.


Lakini pia amefafanua kwamba Kuna miradi ya visima virefu inayotekelezwa katika kata za Tungamaa, Mwera eneo la Mzambarauni, Bweni, Mikinguni kijiji cha Stahabu na kata ya Ubangaa katika kijiji cha Meka.

Post a Comment

0 Comments