Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MGUMBA-CRDB WEKEZENI KWENYE MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakutugenzi wa Benki ya Crdb, Prof. Neema Mori akimpongeza mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba baada ya kuzindua jiwe la msingi katika tawi la benki ya CRDB wilayani Lushoto.
Rc Mgumba akikata utepe ishara ya kufungua rasmi tawi hilo la benki akisa sambamba na viongozi wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa akiongea na wafanyakazi wa Benki hiyo kabla hajaizindua.


********************

Na Hamida Kamchalla, LUSHOTO.

BENKI ya CRDB Mkoa wa Tanga imeshauriwa kuwekeza kwa kutoa mikopo ya miundombinu ya umwagiliaji maji katika mashamba ili kuwaondoa wakulima katika kilimo cha kusubiria mvua na kuwapa uhakika wa kulipa mikopo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba ametoa ushauri huo wakati akifungua tawi jipya la benki hiyo katika Wilaya ya Lushoto ambapo alisema mbali na mikopo mingi inayotolewa na benki hiyo, ni vema wakiwatoa wakulima kwenye kilimo cha kutegemea mvua na kuwapatia miundombinu ya umwagiliaji.

Aidha amesema kuwa, taasisi nyingi zinatoa mikopo kwenye sekta ya kilimo na kuongeza mnyororo wa thamani lakini bado zinatakiwa kuongeza jitihada za kuhakikisha wanaondoa matatizo yanayotokana na kilimo cha kutegemea mvua.

"Ukimkopesha mkulima wa kawaida ambaye hatumii mfumo wa umwagiliaji bado hawezi kunufaika kwa sababu hautakuwa na uhakika kama ukimkopesha mwakani atalima na mvua itanyesha au haitanyesha, na kama isiponyeaha kama mwaka huu ina maana huo ulipaji wa mkopo utakuwa mgumu"

"Rai yangu kwenu, angalieni sera na mikakati y, badala ya Ile mikopo kuanzia kwenye magala ya kutunza mazao, biashara na ununuzi wa mazao, sasa anzeni kutatua tatizo hili la maji, nendeni katoeni mikopo kwenye miundombinu ya umwagiliaji, maana yake mnajibu Ile shida ya mvua, badala yake mkulima atalima zaidi ya mara mbili kwa mwaka mzima" amesema.

Aidha Mgumba ameitaka benki hiyo pia kutoa mikopo kwa Wajasiriamali wadogo bila kuwapa masharti magumu ili nao waweze kuipata na kukuza mitaji yao ambayo itakuwa kutokana na usaidizi kwakuwa hawezi kujitosheleza kwa mitaji yao midogo waliyonayo.

"Pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali na mashirika mengine ya fedha, bado tumeona hawa wajasiriamali wanatakiwa kuwezeshwa ili kukuza mitaji yao, utegemezi wa mitaji yao wenyewe haitoshi kuuza biashara zao" amesema.

"Mara nyingi taasisi za fedha mnasema fedha zipo lakini wajasiriamali wadogo wakija kuomba wanapata usumbufu mwingi kwakuwa hawana dhamana kutokana na masharti yane kuwa magumu, wapo wengine wamesoma wanataka kuanzisha biashara zao hawana mitaji, wale angalieni hata vyeti vyao vinaweza kuwa kama dhamana ili muweze kuwapa mikopo" amesisitiza Mgumba.

Mgumba pia ametoa rai kwa wakulima pamoja na wajasiriamali kuchamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa kuweka akiba na kukopa kwani pia itasaidia kukuza pato la Taifa lakini kujenga uaminifu kwa kukopa na kurejesha fedha kwa ajili ya kupatiwa wengine wenye mahitaji.

"Nitoe rai kwa wakulima wote kuchangamkia fursa hii katika benki ya CRDB, kuchukua mikopo lakini pia kujenga tabia ya uaminifu katika kurudisha mikopo yenu, na mkifanya hivi ni imani yangu tutakopesheka" amebainisha mkuu hiyo.

Hata hivyo ametoa pongezi kwa benki hiyo kwa kuwa kinara nchini katika kupunguza riba ya mikopo yake kwa wananchi kutoka asilimia 21 hadi kufikia asilimia 9.

Naye Ofisa Mkuu Biashara wa Crdb Boma Rabala, amesema benki hiyo imeweka mkakati wa kuwainua wakulima katika suala zima la kuwapatia mikopo ili waweze kuzalisha kwa tija lakini pia amefafanua kwa upande wa wajasiriamali watapatiwa mikopo kwakuwa tayari benki hiyo imepunguza baadhi ya masharti magumu pamoja na riba zake.

"Tumedhamiria kuwapa mikopo wakulima kwa sababu Crdb ina mikakati ya kuwainua ili wafanye kilimo chenye tija lakini pia tumepunguzwa riba zetu na baadhi ya masharti ambayo yatamuwezesha wajasiriamali kupata mikopo na kukuza mitaji yao" amebainisha Rabala.

Baadhi ya wateja wanaotumia benki hiyo wanayoishi wilayani humo walisema wamefurahishwa na kitendo cha kuwekewa tawi hilo karibu kwakuwa walikuwa wakipata tabu kwa kufuata huduma nje ya Wilaya na kusema kwa sasa garama walizikuwa wakipata hazitakuwepo.

"Hapa sasa kwetu watumiaji wa Crdb tumepatta nafuu kubwa, hiki ndicho kulikuwa kilio chetu cha muda mrefu kwani kama mimi nilikuwa nasafiri kwenda Tanga mjini kabisa maana ndiko nilikoanza kufunguliwa akaunti yangu, tunawashukuru sana kwa kuona umuhimu wetu sisi kama wateja wao" amefafanua Ramadhani Mshama.

Post a Comment

0 Comments