Ticker

6/recent/ticker-posts

MASAUNI ATAKA MIPAKA YA KUINGILIA BAHARINI ILINDWE, WANANCHI WATOE USHIRIKIANO KWA SERIKALI.

Waziri Masauni kushoto na mkuu wa Wilaya Surumbu wakiongea na wananchi wa Moa.
Waziri Masauni akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya, wa kwanza kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Sebastiano Masanja.
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu akitoa taarifa ya usalama wa Wilaya hiyo mbele ya Waziri Masauni.
Waziri wa Mambo ya Ndani Hamadi Masauni akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mkinga mara baada ya kuwasili wilayani humo.

********************

Na Hamida Kamchalla, MKINGA .

WANANCHI wanayoishi ndani na nje ya mwambao wa bahari kwenye malango ya kuingilia baharini wametakiwa kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuzuia hali ya uhalifu kuingia nchini wakiwemo wahamiaji haramu.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni alipotembelea katika Bandari ya Moa wilayani Mkinga Mkoa wa Tanga ambapo akiongea na wananchi na kusikiliza kero zao.

Awali akiongea na wananchi hao, alisema kwa kawaida bandari yoyote ni malango ya kuingilia kwenye nchi, hivyo usalama wa Bandari au maeneo yake huwezi kuutofautisha sana na usalama wa nchi, kwani kitu chochote kibaya au wahamiaji haramu wakiingia madhara ni makubwa kwa Taifa.

"Kwahiyo tuna wajibu sisi wananchi tunaoishi katika maeneo haya ya malango ya kuingilia kwenye nchi, yaliyo rasmu na yasiyo rasmi kuweza kushirikiana na serikali yenu kwa namna mbalimbali kudhibiti hali ya uvuniifu wa amani unaoweza kusababishwa katika Taifa letu, na wahamiaji haramu wanaoingia bila kufuata sheria" alisema.

Aidha alifafanua kwamba serikali imejenga Chuo cha jeshi la Uhamiaji wilayani humo kwakuwa umeona jeshi hilo litaweza pia kusaidia katika harakati za kupambana na wahamiaji haramu hivyo hususani katika maeneo hayo yaliyoki kwenye malango ya bahari.

Masauni alibainisha kwamba kwa mara ya kwanza serikali imetoa fedha nyingi katika ujenzi wa Chuo hicho ambapo awali kabla Uhamiaji haijatoka kwenye Idara hakukuweza kujengwa chuo cha mafunzo kama kilichojengwa wilayani humo.

"Nadhani mmemuona Rais wetu Samia Sulluhu Hassan amekuja hapa kuzindua Chuo cha mafunzo ya kijeshi ambapo kwa mara ya kwanza Uhamiaji imekuwa jeshi na mmebahatika ninyi watu wa Mkinga Chuo hiki kutakuwa kiko katika eneo lenu"

"Mama ametoa fedha nyingi sana, kwahiyo tuna Imani kwamba Chuo hiki kitawasaidia pia Wanamkinga, kwasababu kwanza Chuo kile kitaongeza usalama, kwamba askari watakuwa wanakuja hapa kwenye mafunzo, ulinzi utakuwepo kwenye eneo la kule lakini pia utagusa katika maeneo yenu" alibainisha.

Hata hivyo alielezwa kwamba katika suala la maendeleo serikali inajitahidi kusimamia vema miradi katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimi kwa uhakika na ukaribu zaidi katika maeneo yao.

Awali wakiongea kero zao wananchi hao walisema kwa sasa kinachowasumbua ni mitandao ambayo inaingiliana na kiasi na nchi jirani ya Kenya pamoja na wahamiaji haramu ambao kwasasa wameanza kudhinitiwa.

Post a Comment

0 Comments