Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA UJERUMANI BADO INAENDELEA KUKUMBUKA TANGA BAADA YA MIAKA 100 KUJENGA HOSPITALI YA BOMBO

Naibu Waziri wa Ujerumani akisalimiana na wananchi waliokuwa kupata huduma katika hospitali ya Bombo.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akionesha na kutokea maelezo kwa mojawapo ya jengo katika hospitali ya rufani ya Bombo kwa Naibu Waziri pamoja na baadhi ya Wabunge kutoka nchini Ujerumani.

*******************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

SERIKALI nchini Ujerumani bado inaendeleza kuikumbuka hospitali ya Bombo mkoani Tanga katika huduma muhimu za afya baada ya miaka 100 tangu nchi hiyo ilipojenga hospitali hiyo.

Kumbukizi ya ujenzi wa hospitali hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati Naibu Waziri, Shrikisho, Wizara ya Uchumi, Ushirikiano na Maendeleo nchini Ujerumani na baadhi ya wabunge wa nchi hiyo walipotembelea katika hospitali ya Bombo.

Waziri Mwalimu amesema hospitali Bombo ilijengwa na Wajerumani miaka 100 iliyopita lakini bado serikali ya Ujerumani inatoa fedha nyingi nchini katika kusaidia sekta ya afya ambapo hospitali hiyo ni moja kati ya zinazopata fedha hizo kwa ajili ya kuboresha huduma.

"Wanatuoatia fedha kwa ajili ya kuimarisha huduma ya afya ya uzazi, mama na mtoto na wametembelea wodi ya wazazi na wodi ya watoto wachanga mahututi, lakini pia zinatumia hizo fedha kwa ajili ya kuimarisha mapambano yetu dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 na ndio maana tumefungua kituo hiki cha kupima ugonjwa huu" amesema.

Aidha amebainisha kwamba kabla ya kufungua kituo hicho, katika hospitali hiyo walikua wanachukua sampuli na kuzipeleka Dar es salaam kwenye maabara yao kuu ya Taifa ya afya ya jamii na majibu yanarudishwa tena baada ya saa 48 hadi siku tatu.

"Lakini sasa hivi baada ya hii maabara ya kupima Uviko 19 hapa Bombo kwa kutumia kipimo cha PCR kufunguliwa, mtu akipima ugonjwa huu majibu yanaweza yakatoka mapema ndani ya saa 8, kwahiyo hata kama mtu ana safari ya kwenda Mombasa anapima siku hiyo na anasafiri" amefafanua.

"Kwahiyo kwa niaba ya serikali ya Rais Samia Sulluhu Hassan tunaishukuru serikali ya Ujerumani kwa kuendelea kusaidia sekta ya afya nchini kwetu, kwenye huduma ya afya ya mama na mtoto pia wanatusaifia kulipa bima ya afya kwa wakina mama wajawajazito, lakini pia kwenye mapambano dhidi ya ukimwi, kifua kikuu na malaria" amebainisha.

Naibu Waziri wa Shirikisho, Wizara ya Uchumi, Ushirikiano na Maendeleo nchini Ujerumani (BMZ) Dkt. Barbel Kofler akiwa ameambata na baadhi ya wabunge kutoka nchini humo alisema serikali yake inasaidia kutetea wanawake kupitia sera ya usaidizi na maendeleo endelevu katika afya ya mama na mtoto.

"Kwa pamoja tumetembelea kituo cha afya cha Ngamiani na hospitali ya rufani ya Bombo ambazo zinapata msaada kutoka serikali ya Ujerumani kupitia GIZ na KfW, kwa muda mrefu sana serikali yetu imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya, kwa wafanyakazi wa afya, vifaa tiba pamoja na vitu mbalimbali" amesema

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii Medard Beyanga amesema sisi tunaomba kama hii bado ni fursa kwetu kwasababu tunaendelea na mpango wetu wa. maabaraza Uviko 19 kwa kutumia kipimo cha PCR

"Hapo nyuma hospitali hizi zilikuwa zinapeleka sampuli katika maabara kuu lakini sasa serikali ya Rais Samia Sulluhu Hassan inafanya jitihafa za kuongeza upimaji kupeleka karibu na wananchi, vituo vingine vimeshafunguliwa na hiki cha Bombo tumeshakifungua leo na kitatumika kuwasairia wananchi wa Mkoa wa Tanga, kuliko kusubiri majibu kutoka Dar es salaam sasa watapata hapahapa" amefafanua.

Post a Comment

0 Comments