Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKURUGENZI WAMETAKIWA KUANDAA MASHAMBA DARASA KATIKA HALMASHAURI ZAO.


**********************

NA FARAIDA SAID, MOROGORO.

Wakurugenzi wa Halmashauri za mikoa ya Pwani,Tanga Dar es Salaam na Morogoro zinazounda kanda ya mashariki ya maonesho ya Nanenane wametakiwa kuanda mashamba darasa katika maeneo yao ili kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi waliokosa kushiriki katika ngazi ya kikanda na wao wajifunze kwa lengo la kuongeza uzalishaji wenye tija.

Wito huo umetolewa mkoani Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bwana Ghaibu Lingo alipotembelea maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki ambpo aliwataka wakurugenzi kupitia kwa maafisa ugani kupeleka kwa wakulima, wavuvi na wafugaji teknolojia za kilimo,mifugo na uvuvi zinazooneshwa kwenye maonesho ya nanenane waliopo kwenye halmashauri zao.

“Halmshauri nyingi wanaandaa vipando kama sehemu ya kufundishia na mshindano lakini wanavyorudi kwenye maeneo yao hawana maandalizi yanayomfanya mkulima aliekosa kuja kujifunza kwenye maonesho ya nanenane ajifunze kulekule kwenye Halmashauri zao.” Alisama Dc Lingo.
Aidha aliwataka wakulima, wafugaji na wavuvi waliopata fursa ya kutembelea maonesho ya nanenane kutumia ipasavyo elimu walioipata kutoka kwa wataalamu ili kuongeza tija katika uzalishaji wao.

Akiwa kwenye banda la Halmashauri ya Mji wa Kibaha Dc Lingo alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Mshamu Munde kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kuhakikisha vipando vinavyoonesho kwenye banda hilo vinaakisi uhalisia wa mazingira ya wakulima, wavuvi na wafugaji licha ya kusimamishwa kwa maonesho hayo kwa muda.

“Kama kusimamisha nanenane tulisimamisha wote kwa nini wengine wawe juu wengine wawe chini lazima kunamikakati iliyotofautiana na ndio maana matokea yanatofautiana pia kwaiyo ni wapongeze Halmashuri ya Mji wa Kibaha hongereni sana.” Alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Bi.Ngollo Nmlenya ameipongeza Bodi ya Pamba kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhamasisha wakulima wadodogo kwenye Wilaya ya Ulanga na Mkoa mzima wa Morogoro kulima zao hilo ili kuongeza uzalishaji.

Alisema kutokana na kuwepo kwa mwekezaji na mnunuzi wa zao la pamba kumetoa fursa kwa wananchi wa Ulanga na Mkoa mzima wa Morogoro katika kupata ajira za moja kwa moja kupitia kilimo cha zao hilo hali itakayoongeza kipato chao na taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwenye banda la Bodi ya Pamba kwenye maonesho ya nanenane kanda ya mashariki mwekezaji na mnunuzi wa zao la pamba Bwana Vitus Lipagila alisema amedhamilia kurudisha kilimo cha zao la pamba katika kanda ya mashariki ambayo inajumuisha mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Kilimanjaro na Iringa.

Pia aliishukuru Bodi ya Pamba kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kipindi chote ambacho alionesha nia ya kuwekeza kwenye zao la pamba kwa lengo la kuwasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika.

Nae Meneja wa huduma za usimamizi Bodi ya Pamba nchini Bwana Mwanguluma Emmanuel alisema Bodi hiyo imejipanga kuongeza uzalishaji ili kufikia malengo ya serikali ya kufikia tani milioni moja ifikapo 2025.

Alisema ili kufikia tani milioni moja ni lazima kuongeza eneo la uzalishaji wa zao hilo ambapo tayari wameanza kutoa hamasa kwa wakulima wadogo katika mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Kilimanjaro na Iringa.

Post a Comment

0 Comments