Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI ATEMBELEA KIWANDA CHA DZ CARD AFRICA LTD MABIBO


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Jim Yonazi akisaini kitabu Cha wageni mara baada ya kuwasili alipotembelea Kanda maalumu ya Kiuchumi ya Benjamin William Mkapa Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Jim Yonazi Septemba 09, 2022 ametembelea Kanda maalumu ya Kiuchumi ya Benjamin William Mkapa Mabibo Jijini Dar es Salaam. 

Dr. Jim Yonaz amekagua na kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na Kiwanda Cha Kutengeneza SMART CARD cha DZ CARD AFRICA LIMITED kama anavyoonekana Katika picha mbalimbali akiwa na maafisa wa Wizara hiyo alioongozana nao, Uongozi wa EPZA na kiwanda Cha DZ CARD AFRICA LIMITED. 

Akizungunza mara baada ya kukagua kazi za kiwanda hicho Dr. Jim Yonaz ameahidi kutoa ushirikiano zaidi katika kukuza Teknolojia na Uwekezaji nchini kwa Ujumla ili kuendeleza dhamira Njema ya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya Kukuza Uchumi wa Nchi na Kuongeza ajira kwa Watanzania.

Post a Comment

0 Comments