Ticker

6/recent/ticker-posts

MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI


******************

Ndugu Wanahabari, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo ya kuwahamisha baadhi ya Makamanda wa Polisi, ambapo amemhamisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya kwenda Makao makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Benjamini Kuzaga.

Pia, IGP Wambura amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) George Katabazi kutoka Makao makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Benjamini Kuzaga aliyehamishiwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.

Ndugu Wanahabari, Mabadiliko haya ambayo yalianza tarehe 08.09.2022 ni katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi.

Post a Comment

0 Comments