Ticker

6/recent/ticker-posts

MAJALIWA MGENI RASMI KONGAMANO LA SITA LA UWEZESHAJI,DODOMA.


Na Zena Mohamed,Dodoma.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la sita la uwezeshaji Wananchi kiuchumi ambalo litafanyika Septemba 19 Mwaka huu Jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa jijini hapa Septemba,16,2022 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ujio wa Kongamano hilo ambalo litahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali.

“Nitoe wito kwa wananchi wa Dodoma wajitokeze kuhudhuria katika kongamano hili ambalo litakuwa ni fursa kwao katika masuala ya uwekezaji na kama tunavyofahamu kwa sasa hapa makao makuu kwahiyo tujitokeze kwa wingi,"amesema Senyamule.

Amesema kuwa Dodoma ina miradi mingi ya uwezeshaji kiuchumi ikiwamo ya ile ya kilimo cha umwakigili ambacho vijana wengi wamejiingiza katika kilimo hicho huku akisema kuwa jijini hilo ni salama kwenye uwekezaji.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Beng’i Issa ametaja lengo la Kongamano hilo kuwa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Amesema fursa nyingi zitapatikana katika kongamano hilo pamoja na kuwepo kwa majadiliano katika majopo mbalimbali likiwemo jopo la majadiliano la wakuu wa Mikoa na lingine ni la wataalam wa masuala ya uwezeshaji wa uwekezaji nchini.

"Kongamano hili ni muhimu na la pekee ambalo nchini inaenda kukaa kujitathimi katika sera yao uwezeshashaji wananchini kiuchumi hivyo kutakuwa na taarifa ya mwaka ya ambayo inaonesha wananchi walivyowezeshwa,

“Vile vile Kutakuwa na tuzo ya mjasiriamali bora,Taasisi bora za fedha, natoa fursa hii kuwakaribisha sana na tunaamini watu wengi watakuja Dodoma na kwa wale ambao hawatafanikiwa kuja watatzama kongamano hili mbashara,”amesema Katibu huyo mtendaji.

Naye Meneja wa Benki ya Stanbic Dodoma, Oppi Igolola amesema wao kama washiriki wa kongamano hilo wameona ni fursa kwao Kama benki kushiriki katika mijadala ya ya kuchanganua ni namna gani wanaweza kuwawezesha wananchi ili waweze kushiriki katika fursa za biashara na uwekezaji.

"Nalipongeza Baraza hili kwa kuandaa jukwaa hili la kiuchumi lenye malengo ya chanya katika kuwawawezesha Watanzania kunufaika na fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa Taifa letu,"amesema Igolola.

Ameeleza kuwa Benki ya Stanbic inaunga mkono juhudi za serikali katika kuchochea maendeleo huku akisema hivi karibuni wanatarajia kuzindua kampeni inayolenga kuwawezesha wajasirimali kutumia fursa zitokananazo na huduma za kibenki.

Post a Comment

0 Comments