Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUACHANA NA IMANI POTOFU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango kushoto akizundua jengo la mama na mtoto jana lililojengwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango akizungumza na wananchi jana kwenye uzinduzi wa jengo la mama na mtoto lililojengwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Jengo la mama na mtoto lililopo kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure lililozonduliwa jana na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango lililojengwa kwa sh Bilioni 12.9 hadi kukamilika kwa ujenzi.
Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jijini Mwanza wakimsikiliza Makamu wa Rais Dk Philip Mpango wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa jengo la mama na mtoto lililojengwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.


************************

Na Sheila Katikula,Mwanza


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mipango amewataka wananchi kuachana na imani potofu ya matumizi ya chakula wakati wa ujauzito.

Hayo amesema leo wakati akizungumza na wananchi kwenye uzinduzi wa jengo la mama na mtoto la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya Kanda ya Sekou Toure lililopo jijini Mwanza.

Amesema ni vema kuhakikisha mama na mtoto anapata lishe bora kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

"Mtoto akipata lishe bora anaepuka magonjwa ya mara kwa mara na itasaidia kupunguza gharama ambazo zingetumika kwenye matibabu.

Amesema ni vema kuchukua hatua ili baada ya miaka ijayo kuwa na taifa lenye watu wenye uwezo wa kufikili na kufanya kazi kwa tija.

Amesema upatikanaji wa huduma za afya kwa mama na mtoto bado ni changamoto licha ya jitihada za serikali kuhakikisha zinapatikana kwa watanzania wote.

Hata hivyo ameongeza kuwa serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya afya nchini kwa kusogeza huduma kwa wananchi hasa wa kijijini.

Aidha ameipongeza Wakala wa majengo Tanzania (TBA) kwa kusimamia ujenzi wa jengo hilo na kupelekea kukamilika Kwa wakati na kuanza kutumika.

Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure Dk Bahati Msaki amesema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2017 na limeghalimu sh Bilioni 12.9 hadi kukamilika kwa ujenzi huo.

Amesema jengo hilo limeanza kutoa huduma mwezi juni mwaka 2012 kwani mradi huo utaboresha huduma ya afya kwa wananchi wakiwamo wakina mama na watoto.

Mradi huo umeboresha huduma kwa wananchi hususani mama na Mtoto katika Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani pamoja na kufanyika maboresho eneo la kazi kuongeza hazi.

Amesema jengo hilo litapunguza msongamano wa wagonjwa uliopo awali vitanda vilikuwa 140 na hivi sasa vipo 261 vimepatikana hivyo kupelekea kuwa 591.

Amesema uwepo wa jengo hilo litasaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto ambapo jengo hilo tangu lianze kutoa huduma limehudumia wananawake 1883 na watoto 800 .

Hata hivyo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Daud Kondoro amesema wameshiriki kwenye ujenzi huo kwa kutoa ushauri elekezi.

"Tumeshiliki katika kubuni ,kisanifu na kujenga mpaka kumalizika kwa jengo hili na tumefanya ubunifu wa kupima udongo katika eneo hili ili jengo liwe na uimala wa kutoa huduma inayotakiwa," amesema Kondoro.

Amesema katika ujenzi na ubunifu wamezingatia mambo muhimu ili kuhakikisha huduma mbalimbali zinapatikana ikiwamo maji kwani kuna tanki la maji linaloweza kutoa huduma muda wote.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amesema jengo hilo ni miradi mkikubwa inayotekelezwa na serikalia na itakayowasaidia mama wajawazito.

Amesema kuwa katika kuimalisha utoaji wa huduma za afya kwa Mkoa wa Mwanza umepokea jumla ya sh Bil. 37,963,174500, za utekelezaji wa maendeleo.

Aidha ameeleza kuwa Mkoa ulipokea sh Bilion 600,503,800 kupitia mad kwa ajili ya huduma za kununua dawa na vifaa tiba.

Post a Comment

0 Comments