Ticker

6/recent/ticker-posts

MGUMBA ASEMA ATAANZA NA OPERESHENI 'MAPAPA'

Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Luteni Maulid Surumbu alifafanya jambo kwa Mkuu wa Mkoa Mgumba wakati wakiwa kwenye moja ya fuso lililobeba mzigo huo.

Marobota ya vitenge yaliyokamatwa.

Vijana wakipakua mzigo wa vitenge kuushusha katika eneo la kuhifadhia katika kituo cha mpaka wa Horohoro.
Mgumba akikagua mzigo wa vitenge vilivyokamatwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba akiongea na wafanyakazi wa TRA Forodha I katika mpaka wa Horohoro kuhusiana na mizigo kupitishwa kimagendo.


************************

Na Hamida Kamchalla, MKINGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba amesema serikali mkoani humo sasa inakwenda kushuhulika na wafanyabiashara sugu wa mali za magendo yanayopitishwa kinyemela katika mpaka wa Horohoro, wilayani Mkinga.

Mgumba ameyasema hayo baada ya shehena nyingine ya vitenge yenye marobota zaidi ya 180 kukamatwa katika mpaka wa Horohoro juzi, ambapo alisema ana taarifa za wahalifu wote mkoani humo hivyo hakuna muhalifu hata mmoja ambaye yuko salama.

"Siku zote tulizoea tunakwenda kushuhulika na vidagaa, yaani kama ni biashara ya dawa za kulevya tunawashuhulikua wavutaji tu wauzaji tunawaacha, lakini sasa tunakwenda kushuhulika na mapapa ambao walikuwa wanafanya biashara hawakamatiki" amesema.

"Niliwahi kutoa wito hapa mpakani kwamba kila mmoja atubu, sikuja hapa kufikia makabiri, nimekuja kumsaidia Rais kuwatumikia wananchi wa Tanga, kwahiyo mimi nitaendelea kutekeleza maagizo yake katika kusimamia maendeleo, lakini pia kulinda mipaka yetu ili kuondoka vitendo vyote vya kihalifu" ameongeza

Naye mkuu wa Wilaya ya Mkinga Luteni Maulid Surumbu amesema baada ya kupata taarifa za kiintelijensia, kwa kushirikiana na jeshi la ulinzi walianza kufuatilia na kubaini magari mawili aina ya fuso yakiwa na vitenge hivyo ambavyo vilibainika kusafirishwa kimagendo na madereva wa magari hayo wanashikiliwa kwa mahojiano.

Kanali Surumbu amebainisha kwamba kazi hiyo walianza majira ya saa mbili hadi saa tano asubuhi na kukuta magari hayo katikati ya mapori umbali wa km 13 kutoka barabara kuu na km 40 kutoka Tanga jiji.

"Tumejiridhisha kuwa mzigo huu ni wa magendo kwa sababu Haina nyaraka halali ambazo zinaonesha umelipiwa kodi na hauoneshi mahala unakokwenda, lakini pia hata upakiwaji wake waliotumia inaonesha siyo halali kwani wamepanga vitenge chini kisha juu wakaweka mawe aina ya Tanga stone" amefafanya

"Kwahiyo inaonesha kwamba, watu hawa wanaojihusisha na shuhuli hii wana lengo madhubuti kuhakikisha wanakwepesha serikali yetu isipate kodi" ameeleza Kanali Surumbu.

Kaimu Meneja wa Forodha mpaka wa Horohoro Nassor Ibrahim amebainisha kwamba uchepushaji wa mizigo unaitia hasara Mamlaka na serikali kwa sababu mizigo yote inayopita pembeni inakwepa kodi kwa asilimia 100.

"Ni hasara kubwa na inarudisha nyuma maendeleo ya nchi, ni vema wafuate taratibu za nchi, wapite kwenye vituo halali vya kulipia kodi walipie, kwa sababu vinginevyo watapata hasara kubwa" amefafanua Ibrahim.

Post a Comment

0 Comments