Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA YASHAURIWA KUCHANGIA MFUKO WA GLOBAL FUND



***************

Na Magrethy Katengu

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Health Promotion Tanzania ( HDT) imeishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchangia Mfuko wa Global Fund kama nchi nyingine zinavyoendelea kuchangia fedha.

Akingumza leo na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dkt Peter Bujari ikiwa imebakia siku kadhaa kuelekea siku ya uchangiaji wa Mfuko huo utakaofanyika Septemba 19 hadi 21 mwaka huu nchini Marekani , amesema wakati Sasa umewadia serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iahidi kuchangia kiasi Cha fedha kwenye Mfuko huo kwani nao wamekuwa wakinufaika.

Mkurugenzi amebainisha kuwa Mfuko huo mahususi kwa kupambana na Ukimwi,Kifua Kikuu na Malaria umeleta mafanikio makubwa Kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania licha ya kupata msaada wa kutoka kwenye Mfuko huo umefika wakati Tanzania na Nchi zingine za Afrika ambazo hazichangii Mfuko huo ziahidi kuchangia kwa awamu hii ya saba .

"Niseme kuwa kwa Afrika pekee nchi kama South Africa,Kenya,Benini,Namibia,Senegal,Lesotho,Cote D'Ivoire,Togo,na Zimbabwe,zimekua mstari wa mbele katika kuhakikisha nazo zinachangia Mfuko huo,pia hivi karibuni Uganda iliahidi kiasi cha Dola za kimarekani milioni 6 hivyo tunaishauri nchi isiyochangia nayo ichangie"amesema Dkt Peter

Sambamba na hayo amesema kupitia taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HDT Bujira imesema kuwa kidunia Mkutano Mkuu wa uchangiaji wa Mfuko kwa awamu ya saba utafanyika nchini Marekani kuanzia tarehe 9 - 21 Septemba 2022 ,fedha hizi zinategemea kuokoa maisha ya wanadamu zaidi ya milioni 20 Duniani kote ifikapo mwaka 2026.

"Kama ilivyotajwa hapo juu Kwa miaka mitatu 2024-2026 kiasi kinachohitajika ni Dola za kimarekani Bilioni 130 .2,ambapo Mfuko wa Global Fund watachangia Dola za Marekani Bilioni 18 sawa na asilimi 14,vyanzo vya ndani Dola za Marekani bilioni 85.6 "amesema Dkt Peter

Sanjari na hayo Mkurugenzi amesemaWafadhili mbalimbali wa Mfuko wa Global Fund wameahidi kiasi Cha Dola za kimarekani Bilioni 17 .5 ambapo mpaka sasa kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 16.6 zimeisha kusanywa kati ya dola za kimarekani Bilioni 18 sawa na asilimia 92 zinazohitajika." amesema Bujari.

Aidha amesema kuwa kwa Muda mrefu serikali ya Tanzania imekuwa ikishirikiana na Mfuko wa kimataifa wa kupambana na Maradhi ya UKIMWI ,kifua Kikuu na Malaria katika kupanga na kutekeleza afua mbalimbali za kupambana na Maradhi hayo ambapo Global Fund ni Moja ya wafadhili wakubwa Duniani na Kwa nchi ya Tanzania katika kufikia malengo ya sasa ya kutokomeza maambukizi mapya ya kifua Kikuu na virusi vya UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Aidha Michango ya Global Fund imesaidia kupunguza maambukizi mapya,kuwapatia matibabu wagonjwa na hivyo kupunguza vifo na kuwawezesha wengi kushiriki shughuli za uzalishaji Mali na maendeleo ya nchi kwa ujumla hata hivyo ugonjwa wa kifua Kikuu umeendelea kuwa tishio kubwa nchini na Duniani kote ambapo vifo vitokanavyo na ugonjwa huo .

Post a Comment

0 Comments