Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NAPE MGENI RASMI TAMASHA LA "REJOICE"******************************

Na Iddy Lugendo

WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Kusifu na Kuabudu la Rejoice chini ya kwaya moravian efatha choir, ambalo linakutanisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka Afrika septemba 16, 2022 uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi Habari leo septemba 13, mlezi wa kwaya ya Moravian efatha Yona sonelo amesema; maandalizi yamefikia Asilimia 95 Katika kuelekea siku ya tamasha.

Amsema siku ya kesho kwaya Moravian itaanza mazoezi ya mitambo ya sauti na siku ya alhamisi kwaya ambazo zimealikwa watafanya mazoezi ikiwemo kwaya ya joyous celebration kutoka Afrika kusini.

"Siku ya Tamasha tarehe 16 ya mwezi wa tisa Mgeni Rasmi atakuwa ni waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye"Amesema Yona.

Ameongezea kuwa tamasha la rejoice litaanza kuanzia saa 11 jioni na waimbaji wataanza kuimba mpaka alfajiri ya Tarehe 17 siku ya jumamosi.

Kwa upande wa Usalama siku ya tamasha jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha watu wanakuwa salama muda wote wa tamasha hilo.

Aidha amesema tiketi Bado zinapatikana Katika app ya 'NILIPE' ambazo zinaanzi VIP shilingi milioni moja, laki tano, laki moja, Elfu hamsini na elfu ishirini kwa kawaida.

"Tunawakaribisha watanzania wote Katika Tamasha la kuombea Nchi yetu ya Tanzania na Kwa wengine wanaotaka kununua tiketi uwanjani pia zitapatikana" amasema Yona sonelo.

Post a Comment

0 Comments