Ticker

6/recent/ticker-posts

JUMLA YA MIRADI NANE MKOANI MWANZA INATARAJIWA KUTEMBELEWA NA WAZIRI MKUU

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima akizungumza na waandishi wa habari hapo pichani juu ya ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa.


*****************************

Na Sheila Katikula,Mwanza.

Jumla ya miradi nane iliyopo jijini Mwanza inatarajiwa kutembelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne ya Oktoba 15 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo oktoba 13 juu ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema Waziri Mkuu atakuwa na ziara ya siku nne yenye lengo la kutembelea na kuzindua jengo la huduma ya macho kwenye hospitali ya kanda ya rufaa ya bugando.

Malima amewataka wananchi wa mkoani Mwanza kujitokeza kwa wingi barabarani kumpokea Waziri Mkuu kama ilivyo jadi ya wana Mwanza kuwakarimu wageni.

Amesema Oktoba 16 atakagua maendelo ya ujenzi wa daraja la Magufuli na baadaye kusalimia wananchi wa maeneo ya Busisi na Usagara.

Malima alieleza kuwa baada ya kusalimia wananchi hao ataelekea Bukwimba- wilayani Kwimba kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na baadaye kuzindua jengo la huduma ya macho la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.

Oktoba 17 Majaliwa atakagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo Cha Afya Irugwa na baadaye atakagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Irugwa ambapo baada ya ukaguzi huo, ataelekea kisiwa cha Gana kukagua ujenzi wa zahanati ya Gana hatua ya msingi.

"Siku hiyo hiyo Majaliwa atarejea wilayani Nyamagana ambapo atakagua ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi Nyegezi, na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza Hapa Kazi tu katika Bandari ya Mwanza Kusini,"amesema Malima.

Post a Comment

0 Comments