Ticker

6/recent/ticker-posts

UMEME BWAWA LA MWALIMU NYERERE, WAWEKEZAJI WAITWA MKOA WA TANGA KUFANYA MAANDALIZI.


****************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


SHIRIKA la Umeme Mkoa wa Tanga linawaita wawekezaji kuanza kuandaa jinsi ya kutumia umeme wa uhakika wa bwawa la Mwalimu Nyerere pindi utakapoanza kusambaza mkoani humo.


Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Mahusiano wa TANESCO Mkoa wa Tanga Amoni Michael alisema umeme utakasambazwa ni mwingi hivyo kama hakutakuwa na uwekezaji mkubwa wa viwanda utakuwa hauna watumiaji.


Alifafanua kwamba umeme huo ni mpango mkakati mkubwa wa shirika hilo ambao utasahaulisha kabisa suala la kukatika kwa umeme mkoani humo na kusisitiza wananchi kuanza kujiandaa kwa matumizi.


"Nalizungumzia hili bwawa ili wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu umeme unakokwenda kuzalisha pale zile mega watts 2115 zitakapokamilika tutampa nani kama hatujafanya maandalizi sasa hivi,


"Nasisitiza kwamba watu waanze kujiandaa, kama ni viwanda waanze kujenga kwa sababu sisi tunaweza tukaleta umeme hapa ukawa hauna kazi sababu watu hawajafanya maandalizi" alisema.


Aidha alizungumzia sababu ya kukatika kwa umeme mara kwa mara mkoani humo na kusema kuwa mabadiliko ya tabianchi yanachangia kwa kiasi kikubwa kukatika kwa kwa umeme mara kwa mara katika Mkoa wa Tanga baada ya maji kukauka katika mto Pangani.

Michael alisema kutokana na hali hiyo umeme unaozalishwa haukidhi mahitaji ya watumiaji hivyo shirika linafanya mkakati wa kufanya matengenezo kubosha mitambo yake.


"Shirika linaendelea kufanya miradi mbalimbali, lakini sisi Mkoa wa Tanga kwa sababu tunasambaza umeme, tunatumia muda huo kufanya matengenezo na ndiomaana inatokea maeneo fulani yakiwa na umeme kwengine unakatika, lakini hali ikishatengemaa tatizo hili litaisha kabisa"


"Tunategemea muda siyo mrefu tuwe tumemaliza matengenezo kwenye njia zetu, isije ikatokea tena sababu kwamba hali imekuwa nzuri na mvua zimenyesha halafu watu wanakosa umeme, kwahiyo tumeweka hivyo ili kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana muda wote" alisema.


Aidha alibainisha kwamba mbali na matengenezo hayo lakini pia wanahakikisha wanaweza ulinzi mahususi katika maeneo yao ambayo yamepitiwa na nguzo za umeme kwani matatizo mengine husababisha na shuhuli za kibinadamu ambapo watu hulima karibu na nguzo jambo linalopelekea wakati wa mvuo nguzo hizo kuondoka.


Pia alifafanua kwamba endapo tatizo hilo litaendelea kuwepo shirika limeweka mpango wa kugeuza njia zao na kuchukua umeme kutoka Mkoa wa Arusha ambao utaweza kuongeza upatikana wa uhakika mkoani Tanga.


"Mpango wa kati tulionao sasa, mpaka kufikia mwezi wa kwanza tunatarajia mabadiliko ambayo yatatokea, tutakachoenda kufanya tutachukua umeme kutoka kwenye kituo chetu cha Arusha kama hii hali ya ukatikaji wa umeme itaendelea kuwa hivi" alifafanua.

Post a Comment

0 Comments