Ticker

6/recent/ticker-posts

KIPAUMBELE CHA MKOA CHA TAJWA , SASA UTEKELEZAJI UMEANZA.
****************************

NA.Shemsa Mussa, BUKOBA.


Mkuu wa mkoa Kagera Mhe. Albert Chalamila  amesema atahakikisha mikakati na vipaumbele vya mkoa vinatekelezwa kwa wakati kwa lengo la kuunufaisha Mkoa na wananchi kwa ujumla.

Amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ili mkoa ukue ki uchumi lazima viwepo vipaumbele muhimu vya kuzingatia katikautekelezaji ili kuleta maendeleo ya mkoa na kwa manufaa ya wananchi .


"Niwaambie ndungu zangu waandishi wa habari tangu nimeripoti kuwa mkuu wa mkoa kagera yapita miezi mitatu sasa ,hivo ni lazima kama mkoa tuwe na vipaumbele tutakavyoanza navyo katika utekelezaji "amesema Mhe.Chalamila. 


Aidha amevitaja vipaumbele katika utekelezaji ikiwemo sekta ya kilimo ,sekta ya afya,sekta ya Elimu,sekta ya maji, sekta ya mifugo na uvuvi,Barabara pamoja na ajira kwa vijana .


"Vipo vipaumbele vingi na muhimu sana ila kwa kuanza tutaanza na sekta hizo tutatekeleza kimoja baada ya kingine ,na hapa naamnini mkoa utakuwa kiuchumi na kuwa mkoa wa kuigwa" amesema.

Hata hivyo ameongeza kuwa katika sekta ya kilimo Mkoa utaangazia katika upande wa kilimo cha ndizi huku wakiwapatia wananchi elimu bora ya kuzalisha miche kwa utaalamu kutoka katika vituo maalum ikiwemo kituo cha maruku ,zao la kahawa kuongeza uzalishaji pamoja na viwanda huku mahindi na alizeti amesema kutafuta namna ya kuongeaza rutuba katika ardhi pamoja na kutenga eneo kwa ajili ya kilimo hicho.

Post a Comment

0 Comments