Ticker

6/recent/ticker-posts

MGODI WA WILIAMSON DIAMOND LTD WASAINI MKATABA WA HALI BORA NA TAMICO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (anaefuata), Katibu Mkuu wa TAMICO (katikati) na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakiwa wameshikiria Mkataba wa Hali Bora Baina ya TAMICO na WDL uliosainiwa leo Ijumaa Novemba 04, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akikata utepe kwa ajili ya utiaji saini wa mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited uliofanyika leo Ijumaa Novemba 04, 2022.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi ambao umesainiwa baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited uliofanyika leo Ijumaa Novemba 04, 2022.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungimza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited iliofanyika leo Ijumaa Novemba 04, 2022.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu wa TAMICO (katikati) na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakizungumza jambo katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited iliofanyika leo Ijumaa Novemba 04, 2022.
Katibu Mkuu wa TAMICO na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakisaini mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited leo Ijumaa Novemba 04, 2022.


Katibu Mkuu wa TAMICO na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakionesha mikataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited baada ya kusainiwa leo Ijumaa Novemba 04, 2022.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, Katibu Mkuu wa TAMICO na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakikata keki ishara ya kukamilika utiaji saini wa mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited iliofanyika leo Ijumaa Novemba 04, 2022.
(Picha zote na Samir Salum)


*****


Na Samir Salum, Lango la habari


Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited uliopo Mwadui Mkoani Shinyanga umesaini Mkataba wa Hali Bora na Chama cha wafanyakazi migodini TAMICO wenye lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi.


Hafla ya utiaji saini mkataba huo imefanyika leo Ijumaa Novemba 04, 2022 katika uwanja wa michezo wa Mgodi wa Wiliamson Diamond limited ukishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Sophia Mjema pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.


Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Wiliamson Diamond limited Mhandisi Ayoub Mwenda amesema kuwa alikutana na wafanyakazi na kusikiliza kero zao ambao waliomba ikiwemo kupata mikopo kupitia mabank, kuboreshewa mikataba ya kazi kwa waliokuwa na mikataba ya muda mfupi na kuboreshewa maslahi yao.


Amesema kuwa tayari wafanyakazi wameshaanza mikopo na zaidi ya asilimia 75 ya wafanyakazi waliokuwa na mikataba maalumu imefanyiwa kazi.


Mhandisi Mwenda amesisitiza kuwa ili kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi mgodini hapo ni wajibu kwao kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji ambao utawezesha kuboresha maisha yao, kuchangia jamii innayozunguuka mgodi huo na kuchangia katika uchumi wa Taifa.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema Amewaasa wafanyakazi pamoja na Mgodi wa Wiliamson Diamond limited kuhakikisha kila upande unatekeleza wajibu wake ili kutimiza matakwa ya mkataba huo ikiwemo kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wakiwa kazini, afya na kuboresha maslahi yao.


Rc Mjema licha ya kuupongeza uongozi wa mgodi kwa kusaini mkataba huo amewataka uhakikisha unasajiliwa na Kamishna wa kazi ili uanze kazi mara moja huku huku akiwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa, weledi na kwa uaminifu ili kuongeza uzalishaji hali itakayowezesha kuboreshewa maslahi yao.


Aidha amizitaka Taasisi na makampuni yaliyopo katika Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wafanyakazi wanapewa mikataba, kuwaruhusu kujiunga na vyama vya wafanyakazi, kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na wageni wanaofanya kazi kuwa na vibali maalumu.


Naye Katibu Mkuu wa TAMICO Peternus Rwechungula Amemshukuru Meneja Mkuu kwa kushirikiana na wafanyakazi na kusaini mkataba huo kwani ni Takwa la kisheria na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na kampuni hiyo ikiwemo kufanya majadiliano na kuboresha zaidi mkataba huo.


Pia amewahimiza wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kuweza kupata haki zao, kutambuana na kunadiliana ili kuweza kupata haki zao.


Awali akisoma Risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, Kaimu Katibu wa Tawi la TAMICO WDL, Gatti Raphael kwa mkataba huo amesema kuwa hadi sasa kampuni hiyo imekuwa na Mkataba wa hiari (voluntary agreement) hali iliyopelekea kuanzisha mazungumzo ya kuanzishwa mkataba huo ambao utaboresha maslahi ya wafanyakazi.

Post a Comment

0 Comments