Ticker

6/recent/ticker-posts

MRADI WA HPSS WACHANGIA MPANGO KAZI WA KITAIFA KUHUSU MAPAMBANO DHIDI YA USUGU WA DAWA.


******************

DAR ES SALAAM, 22 Novemba 2022: Wizara za Afya, Mifugo na Uvuvi, na Kilimo kupitia Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu shughuri za Kuzuia Usugu wa Vijidudu Dhidi ya Dawa baridi, kwa kushirikiana na Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya, vyuo vikuu na taasisi za utafiti, wameandaa kongamano, kuanzia tarehe 22 hadi 23 Novemba 2022 jijini Dar es Salaam.


Kongamano hili litafanyika katika Wiki ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya Usugu wa Dawa, ambayo hufanyika duniani kote kuanzia tarehe 18 -24 Novemba kila mwaka.


Kauli mbiu ya Wiki ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya Usugu wa dawa ya mwaka huu ni ‘Pamoja katika Kuzuia usugu wa dawa’ na inalenga kuhimiza ushirikiano wa sekta mbalimbali ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya usugu wa dawa.


Shirika la Afya Duniani (WHO) lilianzisha Wiki ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya usugu wa Dawa ili kuelimisha umma, wafanyakazi katika sekta ya afya na watunga sera kwa ujumla matumizi sahihi ya dawa ili kuondokana na kuibuka na kuenea zaidi kwa magonjwa kutokana na usugu wa dawa.


Kongamano hili litakuwa na matukio makuu matatu, ambayo ni: uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Utekelezaji shughuri za mapambano dhidi ya usugu wa dawa (2023-2028), Maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa kuhusu elimu juu ya usugu wa dawa na Kongamano la mapambano dhidi ya usugu wa dawa.


Usugu wa dawa ni mojawapo wa matishio makubwa ya afya ya umma duniani ambayo huperekea kuwa vigumu kutibu maambukizi ya magonjwa ya kawaida na hivyo kuongeza hatari ya kuenea kwa magonjwa hayo na vifo.


Kwa miaka mingi sasa, matumizi mabaya ya dawa kwa binadamu, wanyama na mimea, matumizi mabaya ya dawa na kutozingatia maagizo ya wataalam wa afya kuhusu matibabu kumeongeza tishio la usugu dhidi ya dawa ulimwenguni kote.


Madhara ya usugu dhidi ya dawa katika afya na kwenye mifumo ya afya ni makubwa sana kiasi kwamba yanakadiriwa kusababisha takriban vifo 700,000 ulimwenguni kote kila mwaka. Kama hatua sahihi hazitachukuliwa, inakadiriwa kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na usugu wa dawa inaweza kufikia milioni 10 kila mwaka ulimwenguni ifikapo mwaka 2050.


HEALTH PROMOTION AND SYSTEM STRENGTHENING PROJECT (HPSS), DODOMA REGION A PROJECT FUNDED BY THE SWISS AGENCY FOR DEVELOPMENT AND COOPERATION (SDC) IN COLLABORATION WITH THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


Katika juhudi zake za kupambana na usugu wa dawa, serikali iliunda kamati ya kitaifa ya kuratibu shughuli zote za mapambano dhidi ya usugu wa dawa.


Wakati huo huo, serikali kupitia kamati hiyo imekamilisha mapitio ya Mpango wa Kitaifa wa Mapambano Dhidi ya Usugu wa Dawa wa 2017-2022 na imetayarisha mpango mpya wa 2023-2028, ambao unatarajiwa kuzinduliwa wakati wa wiki ya mapambano dhidi ya usugu wa dawa.


"Kongamano la kwanza kuhusu usugu wa dawa nchini liliandaliwa na mradi wa HPSS Tuimarishe Afya mnamo 2017 na likawa na mafanikio makubwa. Sasa, miaka mitano baadaye, tumefurahi kuona kwamba wazo letu la awali sasa limechukuliwa kikamilifu na serikali”, alisema Dk Karin Wiedenmayer, Mtaalamu Mwandamizi wa Afya ya Umma na Dawa katika Mradi wa HPSS.


Dk Wiedenmayer, pia aliipongeza Serikali na wadau wengine kwa jitihada zao kubwa za kushughulikia na kupunguza madhara ya usugu wa dawa nchini Tanzania.


HPSS Tuimarishe Afya ni mradi wa Ushirikiano kati ya Serikali za Uswizi na Tanzania, unaofadhiliwa na Serikali ya Uswizi na kutekelezwa na Taasisi ya Uswisi ya Tropical and Public Health Institute

Post a Comment

0 Comments