Ticker

6/recent/ticker-posts

CHUO CHA BANDARI CHAJIVUNIA KUTOA WATAALAMU BORA NCHINI

Afisa Msajili katika Chuo cha Bandari Pendo Mtinangi akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Tanga katika viwanja vya Bandari kunakoendelea Mashindano ya Shimuta kuhusu umuhimu wa chuo hicho.
Afisa Msajili katika Chuo cha Bandari Pendo Mtinangi akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Tanga katika viwanja vya Bandari kunakoendelea Mashindano ya Shimuta kuhusu umuhimu wa chuo hicho.
Afisa Uhusiano wa Chuo cha Bandari Edda Mmari akizungumza na waandishi wa habari leo.
Afisa Utawala Mwandamizi katika chuo hicho Halima Kagobe akizungumza.
Mratibu wa mafunzo ya muda mfupi John Leonard akizungumza.


Chuo cha Bandari kimejivuna kutoa wataalamu bora wengi ambao wamekuwa ni chachu ya mafanikio katika sekta ya uchukuzi na nyingine hapa nchini.

Hatua hiyo inatokana na takwimu kuonyesha kuwa fursa ya ajira kwa wahitimu wake ni zaidi ya asilimia 90 huajiriwa katika maeneo mbalimbali ya sekta ya uchukuzi Nchini .

Hayo yalibainishwa Leo naAfisa Utawala Mwandamizi katika chuo hicho Halima Kagobe wakati wakizungumza na waandishi wa Habari Jijini Tanga katika viwanja vya Bandari kunakoendelea Mashindano ya Shimuta.

Ambapo alisema kuwa Kutokana na umahiri wa uwepo miundombuni bora ya kujifunza umefanya chuo hicho kuweza kutoa wanafunzi ambao wanahitajika katika soko la ajira.

Alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia ambayo chuo hicho kinakwenda sambamba Kwa kuweka mitambo ya kisasa pamoja masomo ambayo ya yanaendana na hitajio la soko la ajira.

"Chuo chetu kinajukumu la kuandaa wataalamu ambao wataweza kutumika na TPA pamoja na sekta nzima ya uchukuzi kutokana na mafunzo ambayo wanayatoa Kwa Wanafunzi wao"Alisema Kagobe.

Awali akizungumza Mratibu wa mafunzo ya muda mfupi John Leonard alisema kuwa kozi za uendeshaji wa mitambo kwa kipindi cha miaka ya hivi karibu imepata mwitikio mkubwa na vijana wa jinsia ya kike.

Alisema kuwa mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho sio tuu yameweza kunufaisha wananchi wa hapa nchini pekee hadi nje ya nchi hususani zilizoko katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.

"Kwa sasa chuo tumefanikiwa kufunga mashine za kisasa ya kufundishia ambayo inajulikana kwa jina la "Simulation"ambapo imeongeza chachu ya washiriki kujifunza kozi za mashine katika chuo cha Bandari "Alisema.

Alisema pia chuo hicho kinaendesha mafunzo ya utaalamu mbalimbali kama usimamizi wa forodha pamoja na usafirishaji kwa wadau mbalimbali katika sekta ya uchukuzi.

Naye kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Chuo cha Bandari Edda Mmari alisema wameshiriki kwenye mashindano ya Shimuta yanayoendelea Jijini Tanga ili kutangaza chuo hicho ambapo alisema chuo hicho kinatoa mafunzo katika eneo la Bandari hususani shughuli za utekelezaji,usalama,na uendeshaji wa mashine za kupakia na kupakulia mizigo.

Post a Comment

0 Comments