Ticker

6/recent/ticker-posts

UBORESHAJI HUDUMA YA MAKTABA UENDE SAMBAMBA NA MABADILKO YA TEKINOLOJIA.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia Omary Kipanga akiongea na wadau pamoja na viongozi wa Bodi ya maktaba.wakati wa ufunguzi wa kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba, tamasha la vitabu na usomaji lililofanya katika hoteli ya Tangabeach jijini Tanga
Sehemu ya wadau wa Elimu wakifuatilia ufunguzi wa kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba, tamasha la vitabu na usomaji lililofanya katika hoteli ya Tangabeach jijini Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akiongea wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Kitaifa la huduma za maktaba, tamasha la vitabu na usomaji lililofanya katika hoteli ya Tangabeach jijini Tanga

Viongozi na Wakutubi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba, tamasha la vitabu na usomaji lililofanya katika hoteli ya Tangabeach jijini Tanga.


*********************
Na Hamida Kamchalla, TANGA.


SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Takinolojia iko kwenye mchakato wa kurekebisha sera ya elimu ya mafunzo ya mwaka 2014 na sheria ya elimu ya mwaka 1978 ili kuendana na ulimwengu wa sayansi na tekinolojia.


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Takinolojia Omary Kipanga ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba, tamasha la vitabu na usomaji lililofanya katika hoteli ya Tangabeach jijini Tanga na kusema, katika sheria hizo kuna maboresho yanayoendelea ili kukidhi mahitaji ya sasa.


Kipanga amesema duniani kote kumekuwa na ukuaji wa tekinolojia ya habari ambayo imeleta ongezeko kubwa la taarifa na habari kutoka vyanzo mbalimbali vya habari, hivyo kongamano hilo limekuja wakati muafaka ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na tekinolojia.


"Hivyo basi serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Takinolojia nchini ilitoa miongozo kupitia sheria kupitia Bunge ya namba 6 ya mwaka 1975 iliyoanzisha Bodi ya maktaba pamoja na sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978" amesema."Katika mabadiliko hayo, sera hizo ni lazima ziakisi mahitaji kijamii, hivyo mitaala inayoongoza kwa ajili ya mafunzo iongoze pia upatikanaji wa walimu, wakufunzi na wahazili iende sambamba na upatikanaji wa wakutubi mahiri katika kufanikisha muongozo wa walimu nchini" amesema.


Aidha amebainisha kwamba sera ya Taifa ya taarifa na huduma ya maktaba nayo iwepo ili kukidhi mahitaji ya jamii, ambayo ndio ipo mbioni kwenda kuibua maeneo yote ambayo yalisomeka kuwa hayana sera.


Sambamba na hayo amesisitiza kuwa miundombinu na vitendea kazi katika maktaba zote nchini viboreshwe kuanzia barabara shule za msingi hadi vyuo vikuu lakini pia kuwepo na uwekezaji.


"Hivyo nitoe wito, kama ilivyo katika elimu, Bodi ya maktaba nchini iendelee kusimamia ubora wa huduma za maktaba zote katika ngazi zote, kuanzia Wilaya" amesisitiza Kipanga.


Awali akitoa taarifa ya Bodi, Mkurugenzi wa Bodi ya Maktaba nchini Dr. Mboni Ruzegeya ametoa maombi alisema matatizo kadhaa yaliyopo katika Bodi hiyo, ikiwemo uhapa wa wakutubi, lakini pia ukosefu wa majengo.


Dr. Ruzegeya amebainisha kuwa kuna baadhi ya maeneo shuhuli za maktaba zinafanyika katika majengo ya halmashauri jambo ambalo inawawia vigumu kufanya shuhuli zao kwa muda unaotakiwa kutokana na majengo hayo kufungua muda ambao wao wanaendelea na kazi.


"Kama Bodi tunaiomba serikali kutuwezesha fedha kwa ajili ya kuongeza wanafunzi wa maktaba, lakini pia tunaziomba halmashauri kututengea maeneo kwa ajili ya ujenzi wa maktaba ili tuwe tunajitegemea na kufanya shuhuli zetu kwa uhuru" amebainisha.


Naye mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema amepokea ombi la kutenga maeneo lakini suala hilo linarudi wizarani na kusubiria kutolewa muongozo na Waziri mwenye dhamana.


"Tunamuombea Waziri wa Elimu, ni vizuri akatuletea muongozo haraka kutuelekeza ni wapi tunatakiwa tutenge maeneo, sisi tutatekeleza, na hii imekuja ni ombi kutoka kwa Bodi, tukiletewa muongozo mimi nitatoa maelekezo kwenye halmashauri" amesema Mgumba.

Post a Comment

0 Comments