Ticker

6/recent/ticker-posts

*WANAFUNZI ADEM MWANZA WAFURIKA BANDA LA PSSSF

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameagiza sekta ya fedha nchini kuja na ubunifu ambao utaifanya sekta hiyo iweze kuchangia zaidi katika pato la Taifa.

Dkt. Mpango alisema hayo Jijini Mwanza katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyokutanisha taasisi mbalimbali za fedha ikiwemo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, maadhimisho hayo yalianza Novemba 21, 2022 na yanatarajiwa kufikia tamati Novemba 26, 2022.

“Kwa muda mrefu sasa mchango wa sekta ya fedha katika pato la taifa umekuwa chini ya asilimia nne...hatuna budi kubadilisha mwelekeo huu, ukizingatia jitihada mbalimbali zilizowekwa hadi sasa, kwahiyo ninaitaka Wizara ya Fedha na Mipango, pande zote mbili za muungano kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania, Umoja wa Mabenki Tanzania na wadau wote mnaoshiriki maadhimisho haya mfanye tafakuri ya kina kuhusu namna ya kuongeza ubunifu ili sekta hii iweze kuchangia zaidi katika jitihada za kupunguza umasikini na kuogeza maendeleo ya Watanzana”alielekeza Dkt. Mpango.

Katika hatua nyingine: Wanafunzi wa chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) tawi la Mwanza wametembelea banda la PSSSF katika maadhimisho ya wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea Jijini Mwanza na kujifunza huduma mbalimbali za Mfuko ikiwemo huduma ya PSSSF kiganjani.

Idadi kubwa ya wanafunzi hao walifika katika banda la PSSSF kwa lengo la kufatilia uwasilishwaji wa makato yao na waajiri wao,hata hivyo baada ya kupatiwa elimu ya PSSSF kiganjani walivutiwa na wengi wao walielekezwa jinsi ya kutumia huduma hiyo kupitia simu za kinganjani.

“Kwa kweli tunawapongeza PSSSF kwa huduma bora, wengi wetu tulifika hapa kwa lengo la kufatilia michango yetu, lakini baada ya kupatiwa elimu ya PSSSF Kiganjani tumeielewe na wengi wetu sasa tunaitumia na kuanzia sasa tutakuwa tukipata taarifa mbalimbali kupitia simu zetu” alifafanua Bw. Shabban Hamza, Wanachuo wa ADEM.

Huduma ya PSSSF kinganjani inamwezesha Mwanachama na Mstaafu kupata huduma kupitia simu janja bila kuhitaji kufika kwenye ofisi za Mfuko kupata huduma husika. Huduma zinazopatikana ni pamoja na; Taarifa za uchangiaji, Taarifa za malipo ya pensheni, Taarifa kuhusu uanachama na kupata mrejesho wa maswali mbalimbali.

Wakati huohuo: Viongozi mbalimbali watembelea banda la PSSSF katika Wiki ya Huduma za Fedha na kujifunza mambo mbalimbali, viongozi hao ni pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango; Mh. Hamad Hassan Chande, Mkuu wa mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria, Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii katika Wizara ya Kazi, Bw. Festo Fute na Waziri Mstaafu, Mhandisi. Christopher Chiza.

Kwa nyakati tofauti viongozi hao walifurahishwa na uharaka wa huduma za PSSSF zinazotolewa katika ofisi zake zilizopo maeneo mbambali ya nchi.


Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabrieli Zakaria (kulia) akipokea kitabu cha Mwongozo wa Mwanachama kutoka Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi alipotembelea banda la PSSSF katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea Jijini Mwanza.
Waziri Mstaafu, Mhandisi Christopher Chiza (kushoto) akipokea kitabu cha Mwongozo wa Mwanachama kutoka kwa Bw. Michael Bujiba, Meneja kutoka kurugenzi ya Fedha ya PSSSF, alipotembelea banda la PSSSF katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea Jijini Mwanza.
Wanafunzi wa chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) tawi la Mwanza wakiwa katika banda la PSSSF katika maadhimisho ya wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea Jijini Mwanza, wakielekezwa jinsi ya kutumia huduma ya PSSSF kiganjani kutoka kwa Afisa wa PSSSF, Bw. Tabori Mugeta (kushoto).

Post a Comment

0 Comments