Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDUMBARO ATAKA MRADI WA KITUO JUMUISHI CHA TAASISI YA SHERIA KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA

Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro wa kwanza (kushoto) akifungua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la kituo jumuishi cha taasisi za kisheria kilichopo Wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Waziri wa Katiba na sheria Dk Damas Ndumbaro akizungumza na viongozi mbalimbali kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la kituo jumuishi cha taasisi za kisheria kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza
Mkurugenzi wa Huduma za Ushauri kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Wencelaus Kizaba akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo jumuishi cha taasisi za kisheria.
Mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Nyamagana,Flora Magabe ameipongeza Serikali kwa kusogeza huduma kwa wananchi pindi kituo hicho vitakapo kamilika.

**********************


Na Sheila Katikula,  Mwanza


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro ametaka mradi wa kituo jumuishi cha taasisi ya sheria kinachojengwa Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya fedha yenye tija na maslahi kwa nchi.

Hayo ameyabainisha leo wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye jengo la kituo jumuishi cha taasisi za kisheria mkoani Mwanza amesema ujenzi wa jengo hilo unapaswa kuwa kichocheo kwa ujenzi wa majengo mengine Kama hayo katika sehemu nyingine za Nchi.

Dk Ndumbaro ameeleza kuwa ili kuweza kufikia malengo ni lazima wahakikishe wanatembea katika dira na dhima ya wizara na kuendelea kuimarisha miundmbinu katika kuhakikisha uapatikanaji wa haki unakuwa kiurahisi Kwa Kila mtu.

"Kutokana na hili nipende kutoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita imeendelea kutoa fedha kwa mahakama ambapo miradi mbalimbali imeendelea kujengwa ikiwemo ujenzi wa vituo jumuishi katika Mikoa mbalimbali" amesema Dk Ndumbaro.

Hata hivyo amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anakamilisha jengo hilo kwa wakati na ubora kwani fedha zinazotumika ni za wananchi.

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Eliezer Feleshi ameeleza kuwa ujenzi wa vituo jumuishi utasaidia kuwezesha taasisi za kisheria za serikali, Wizara pamoja na wadau muhimu Kwa pamoja kuongeza tija katika kutoa huduma.

Feleshi amesema mpango huo utafanikisha kazi zinazofanywa na mahakama mtandaoni pamoja na kuondoa zinazowakabili katika maeneo yenye mahakimu wengi kuliko mawakili wa serikali.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho Mkurugenzi wa Huduma za Ushauri kutoka Wakala Majengo Tanzania (TBA), Wencelaus Kizaba amesema jengo hilo litagharimu Sh Bilioni 3,181,548,096.83 hadi kukamilika kwa ujenzi huo.

Kizaba amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ulianza aprili 26 mwaka huu na unatarajia kukamilika oktoba 25 mwaka 2023 kwani mpaka hivi sasa upo asilimia 35 ya ujenzi wa kazi zote za mkataba.

Ameeleza kuwa mradi huo umetoa ajira mbalimbali kwa wataalamu na wafanyabiashara wadogo wadogo ,umetoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vya nchini

"Vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi huu vinatoka kwenye viwanda vyetu vya ndani ikiwemo Saruji,Rangi,Mabomba na baadhi vitatoka kwenye viwanda vya nje,"amesema Kizaba.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Nyamagana,Florah Magabe ameipongeza Serikali kwa kuanzisha vituo jumuishi vitakavyosaidia kukabiliana na vishoka.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema wataendelea kushirikiana na Wizara hiyo ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments