Ticker

6/recent/ticker-posts

MAPOKEZI WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR RAIS MWINYI


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Zanzibar Ndg.Dk Ali Mohamed Shein, baada ya kumalizaka kwa sherehe za mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar zilizofanyika katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja Jijini Zanzibar leo 11-12-2022.(Picha na Ikulu)

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kuitikia dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume, iliyofanyika katika kaburi la marehemu viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja leo ikiwa ni sherehe za mapokezi yake akitokea Mkoani Dodoma baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg.Hemed Suleiman Abdulla na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Zanzibar Ndg. Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu) MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja Jijini Zanzibar leo wakati wa sherehe za mapokezi yake akitokea Mkoani Dodoma baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa 10 na kuchaguliwa kwa kura nyingi kwa nafasi ya Makamu Mwenyekitin wa CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments