Ticker

6/recent/ticker-posts

JAJI DKT. JOHN UTAMWA AFARIKI DUNIA


******************

02 Januari, 2023 Dar Es Salaam

Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania, anasikitika kutangaza kifo cha Mhe. Dkt. John Harold Kulimba Utamwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa kilichotokea leo tarehe 02/01/2023 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa anapatiwa matibabu.

Marehemu Mhe. Jaji Dkt. Utamwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la Damu ambapo tarehe 17 Desemba, 2022 alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Mnamo tarehe 18 Desemba, 2022 alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuendelea kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomfika.

Marehemu Jaji Dkt. Utamwa alijiunga na Mahakama ya Tanzanaia tarehe 17/02/1992 akianzia ngazi Hakimu Mkazi. Alipanda ngazi mbali mbali ndani ya Mahakama na hatimaye aliteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 24/6/2010. Akiwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Marehemu Jaji Dkt. Utamwa alifanya kazi katika kanda za Dar es Salaam, Tabora, Mbeya na Iringa.

Kufuatia Msiba huo, taratibu za maziko zinafanyika nyumbani kwa marehemu Madale jijini Dar es salaam. Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitaendelea kutolewa.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Post a Comment

0 Comments