Ticker

6/recent/ticker-posts

MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, HUDUMA YA AFYA LUSHOTO IMEBORESHWA.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Handeni, Dkt. William Machary.

**************************

Na Hamida Kamchalla, LUSHOTO.


FEDHA za miradi ya afya zilizopelekwa katika Wilaya ya Lushoto zamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto waliokuwa boo umbali mrefu kufuata Need katika hospitali ya Wilaya.


Hayo yamesemwa na Msimamizi wa miradi ya ujenzi idara ya afya katika halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Dkt. Shabiru Msumari alipoongea na waandishi wa habari na kusema serikali ya awamu ya sita imetoa kiasi cha sh bilioni 3.78 kwa ajili ya vituo vya afya lakini pia jengo la kisasa la mama na mtoto katika hospitali ya Wilaya.


"Katika kipindi hiki cha miaka miwili, halmashauri tumeupokea sh bilioni 3.78 kwa ajili ya ujenzi mbalimbali ya miradi ya afya, ikiwepo vituo vikubwa vya afya vitatu na zahanati nane, tuna vituo vya afya vya Lunguza na Kwekanga ambako tumepokea takribani sh milioni 800 ambazo ni fedha za tozo" amesema."Lakini pia tuna kituo cha afya cha Mtae ambacho kimepokea sh milioni 400, lakini pia tuna zahanati nane ambazo kila moja imepokea sh milioni 50 kwa ajili ya kumalizia maboma ambayo yapo kwenye hatua mbalimbali na mpaka sasa mengine yanakaribia kutumika" amebainisha.


Alieema awali kabla ya ujenzi huo kufanyika wananchi walikuwa katika hali ya mateso lakini sasa hivi huduma nyingi zitakuwa zikipatikana kule kwenye maeneo yao, kama kule Mtae kituo cha afya kina jengo kubwa la mama na mtoto, ambalo litasaidia kuwapunguzia mwendo kwenda hospitali ya Wilaya.


"Kituo kule kutaleta mapinduzi makubwa sana, wananchi watapunguziwa garama kubwa ya kutembea umbali mrefu zaidi ya km 50 lakini pia wengine kupoteza watoto njiani" amebainisha Msumari.


Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Lushoto, Dkt. William Machary amesema tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo hakukuwepo na jengo maalumu la huduma ya afya ya mama na mtoto lakini kwa sasa uhitaji ni mkubwa sana ndipo serikali ikatenga bajeti.


Dkt. Machary amesema katika mwaka wa fedha 2018/19 serikali kupitia mfuko wa Global Fund ilitoa fedha kiasi cha sh milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali hiyo lakini kutokana na uhitaji mkubwa wa jengo hilo waliomba kubadili matumizi.


"Halmashauri ya Wilaya iliomba idhini kwa Katibu Mkuu TAMISEMI kubadilisha matumizi na kujenga jengo la mama na mtoto ili kuboresha huduma hiyo" anesema Machary.


Vilevile amesema kwa Wilaya hiyo wakina mama wanaokwenda kujifungua ni wengi, na mpaka sasa ni kuanzia 280 hadi 300 kwa mwezi, kwahiyo hali hiyo inaongeza uhitaji mkubwa wa jengo kubwa kwa ajili yao ambalo litahudumia kwa ubora zaidi na kuwapa hali nzuri wakati wa kujifungua.


"Kwahiyo jengo hili jengo hili linakwenda kuondoa kadhia ile ambayo tuliyokuwa tunaiona ya wakina mama wakijifungulia katika sehemu finyu ambayo hata wahuduku wa afya walikuwa wanashindwa kufanya kazi zao kwa uhuru" amesema.


"Pia jengo hili litaenda kusaidia sana kwa maana ni la kisasa zaidi ambapo Lina kila kinachohitajika ndani, lakini pia Lina sehemu ya kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya miezi (njiti), na hata wale ambao wanaozaliwa na matatizo, kwa kifupi lina uwezo wa kutoa huduma zote" amefafanua.


Dkt. Machary ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo ya jirani kuacha tamaduni za zamani kujifungulia majumbani badala yake wafuke hospitalini haraka pindi wanapojihisi wana ujauzito ili kuanza huduma ya kliniki na kujifungulia hospitalini kwa usalama wao na watoto.


Baadhi ya wazazi waliokuwepo hospitali hapo walieleza furaha yao kupatiwa jengo hilo na kudai kuwa awali wengi wakipata adha ya kujifungulia nyumbani ambako haikuwa salama kwao na watoto kwani mara kadhaa waliweza kupoteza watoto au wazazi wenyewe.

Post a Comment

0 Comments