Ticker

6/recent/ticker-posts

MICO YAFANYA KONGAMANO LA KWANZA LA KIBIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM



*******************************

Na Magrethy Katengu

TAASISI ya Kimataifa ya Ithibati (viwango) Mico imefanya kongamano la kwanza la kibiashara jijini Dar es Salaam lenye lengo la kubainisha, kutoa elimu na kuweka wazi masoko ya bidhaa mbalimbali.

Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Skeikh Hamid Jongo ameipongeza Halal kwa kuandaa kongamano hilo kwani itakuwa chachu pekee ya Wafanyabiashara kuona fursa zilizopo na bidhaa zao kuaminika ndani na nje Kimataifa

Sheikh Jongo amesema kuwa uwepo wa Taasisi ya Halal nchini ni jambo jema kwani imekuwa ni kiu ya muda mrefu kwa wafanyabiashara na Serikali.

Hivyo Taasisi hii itasaidia kutoa uthibati kwa bidhaa mbalimbali hivyo kusaidia kupenya katika masoko ya ndani na nje na kuchangia pato la Taifa.

“Pengine tumekuwa tukikosa soko la kuuza bidhaa, hivyo wafanyabiashara bidhaa zao zitathibitishwa kupitia Halal na hivyo kuongeza mapato kwa kwa Serikali,” amesema Sheikh Jongo.

Sheikh Jongo amebainisha kwamba licha ya hayo, ni kwamba itasaidia kupatikana kwa bidhaa bora kama vile za chakula, nguo nyama kwa ajili ya biashara za nyingi za wateja.

Sheikh Jongo amesema kuwa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) linaunga mkono na kupongeza kwa jambo hilo kwani litasaidia Mtanzania kula chakula safi, mavazi safi na hivyo kuwa na maisha mazuri.

Hata hivyo wafanyabiashara wa Tanzania wamekuwa wakienda nchi zingine kwa ajili ya kufata ithibati ya bidhaa zao hivyo Halal itawarahisishia kupata ithibati ndani ya nchi.

“Kwa kupatikana kwa kampuni ya Halal itakuwa rahisi kwa wafanyabiashara kupata ithibati na kufanya biashara ndani na nje,” ameongeza Sheikh Jongo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TanTrade Latifa Khamis amesema kwamba soko la Halal limekwenda kimataifa.

Hivyo kupitia Halal wafanyabiashara watasaidiwa kujua bidhaa halali na zisizo halali ili kuweza kuhimili soko la ndani na nje.

“Hivyo ili wafanyabiashara waweze kufanya vizuri wanatakiwa kijua Halal ni nini, naomba waitumie sana Halal kwani itawapatia ithibati ya bidhaa zao,” amesema Latifa.


Naye Naibu Mkurugenzi wa Mico Halal Muhamed Juma amesema kwamba kongamano hilo ni la kwanza na lengo lake ni kubainisha, kuelimisha na kuweka wazi masoko.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wafanyabiashara na wasio wafanyabiashara lengo kujifunza na kupata ufahamu kuhusu Halal.

Post a Comment

0 Comments