Ticker

6/recent/ticker-posts

MKE WA RAIS MAMA MARIAM MWINYI AFUNGUA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI KWA MCHEZO WA NETIBOLI

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akirusha mpira golini kuashiria kuyafungua Mashindano ya Kombe la Mapinduzi katika uwanja wa Gmkhana Wilaya ya Mjini Unguja leo 4-1-2023, katika mchezo wa ufunguzi ulizikutanisha Timu za KVZ na Zimamoto na Timu ya KVZ imeibuka na ushindi wa bao 42-41.(Picha na Ikulu)MCHEZAJI wa Timu ya Zimamoto Pendo Adrian Mpela akiwa na mpira wakati wa mchezo wao wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya KVZ,uliofanyika katika uwanja wa Gmykhana, Timu ya KVZ imeshinda mchezo huo kwa bao 44 -41.(Picha na Ikulu)

MCHEZAJI wa Timu ya Zimamoto Tatu Ali Mussa akijiandaa kudaka mpira wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Wilaya ya Mjini Unguja. Timu ya KVZ imeshinda mchezo huo kwa bao 44-41.(Picha na Ikulu) MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya KVZ wakati wa ufunguzi wa Michuano ya Netiboli Kombe Mapinduzi uliyofanyika katika uwanja wa Gmkhana Wilaya ya Mjini Unguja leo 4-1-2023.(Picha na Ikulu) MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Zimamoto wakati wa ufunguzi wa Michuano ya Netiboli Kombe Mapinduzi uliyofanyika katika uwanja wa Gmkhana Wilaya ya Mjini Unguja leo 4-1-2023.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments