





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa kimpongeza Ramadhan Omar Mcha Wanamadrasa waliokuwa wakisoma Qaswida kwa Kumshindikiza Rais baada ya hafla ya Ufunguzi wa Masjid Istiqama katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, hafla iliyofanyika leo ambapo Viongozi mbali mbali na Waumini walihudhuria katika sherehe hiyo. [Picha na Ikulu] 13/01/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Masjid Istiqama ,Msikiti uliojengwa Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa Bw.Suleiman Mohamed Yahya (wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman (kushoto) katika sherehe iliyofanyika sambamba na Swala ya Ijumaa leo.[Picha na Ikulu] 13/01/2023. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Mfadhili wa Ujenzi wa Masjid Istiqama Bw.Suleiman Mohamed Yahya mara alipowasili na kufungua Msikiti huo leo,uliojengwa Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.[Picha na Ikulu] 13/01/2023.
0 Comments