Ticker

6/recent/ticker-posts

CHONGOLO AYATAKA MABARAZA YA MADIWANI NCHINI KUFANYA KAZI ZA KUJADILI MASLAHI YA WANANCHI .

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo,Akizungumza na Wananchi wa Kinole wakati msafara wake , ukiwa njiani kwenda Kata ya Tegetelo, kukagua Mradi wa Maji wa Morong’anya.(Picha Zote na Fahadi Siraji CCM)

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi, Ndugu Sophia Mjema,Akizungumza na Wananchi wa Kinole wakati msafara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo , ukiwa njiani kwenda Kata ya Tegetelo, kukagua Mradi wa Maji wa Morong’anya, Kulia ni katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi (Gavu.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi, Ndugu Sophia Mjema,Akizungumza na Wananchi wa Kinole wakati msafara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo , ukiwa njiani kwenda Kata ya Tegetelo, kukagua Mradi wa Maji wa Morong’anya.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi, Ndugu Sophia Mjema,Akishihirikiana na akina mama ntilie kupika chakula katika Kibanda cha Rehema Shomali,wakati msafara Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo ,Uliposimama kuzungumza na wananchi na Kushiriki shughuli za kijamii ukiwa njiani kwenda Kata ya Tegetelo, kukagua Mradi wa Maji wa Morong’anya.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, katikati mwenye kofia akipata chakula na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sofia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu, Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Tale Tale pamoja na wananchi wengine katika mgahawa wa mama lishe katika Kibanda cha Rehema Shomali kata ya Kinole Mororgoro Vijijini akiendelea na ziara yake mkoani humo. Leo tarehe 3 Februari, 2023.(Picha Zote na Fahadi Siraji CCM)

***********************

KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameyataka mabaraza ya madiwani nchini kufanya kazi za kujadili maslai ya wananchi na sio kurumbana kwa maslai yao binafsi.

Katibu mkuu Chongolo alisema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika kijiji cha Kinole, jimbo la Morogoro kusini Mashariki ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tisa Mkoani Morogoro yenye lengo la kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo.

"Madiwani kazi yenu ni kujadili hoja zenye tija na sio kuvutana bila sababu za msingi" alisema.

Alisema amepata taarifa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Hamis Tale kuwa Serikali ilipeleka fedha za kituo cha afya cha Kinole lakini fedha hizo ziliondolewa baada ya kutokea marumbano wapi kituo hicho kijengwe.

"Naenda kuziwekea msisitizo fedha hizo zirudishwe ndani ya miezi miwili fedha zitakuwa zimefika "alisema..

Akizungumzia elimu Chongolo aliwataka wazazi katika wilaya ya Morogoro vijijini kuacha tabia za kuwafundisha watoto mambo ya wakubwa kabla ya umri wao.

"Zamani mtoto wa kike akimaliza darasa la saba anachezwa ngoma kisha anaolewa, acheni kuwafanya watoto wa kike mahari"alisema

Pia aliwataka wazazi hao kuacha kuwageuza watoto kike kuwa wafanyakazi wa ndani na badala yake wawapeleke shule ili waweze kuhudunia familia zao kwa tija.

Kwa upande wa Afya, katibu huyo aliwataka kuacha kujitibu kwa waganga wa jadi na badala yake watumie huduma za vituo vya afya.

"Serikali imewekeza fedha nyingi katika vituo vya afya na hospitali hakuna sababu ya kwenda kutibiwa kwa waganga wa jadi"alisema.

Awali katibu wa shina namba 2 Shomari Mkude alisema katika vikao vyao vya shina hujadili kuhusu masuala ya kilimo na kumuhakikishia Chongolo wanatarajia kuvuna mazao ya kutosha ifikapo mwezi Aprili na hivyo hawatakuwa na njaa.

Pia katibu huyo wa tawi alisema wanamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea madarasa mapya ya kutosha hali itakayowafanya wanafunzi kusoma vizuri .

Katibu huyo wa tawi alitaka kujua kuhusu ujenzi wa barabara ya kutoka Bigwa hadi Kisaki kwa kiwango cha lami unaanza lini.

Akijibu hoja hiyo meneja wa wakala. wa barabara mkoa wa Morogoro Alinanuswe Kyamba alisema Machi 8 watafungua zabuni ya barabara hiyo ambapo kufikia mwezi mwaka huu mkandarasi atakuwa ameanza kazi.

Kwa Upande wake Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu amewasisitiza Wana CCM na wananchi kwa ujumla kuendelea kuzalisha chakula cha kutosha ili kuwa na uhakika wa chakula.

Post a Comment

0 Comments