Ticker

6/recent/ticker-posts

KINANA AWATAKA VIONGOZI CCM KUELEZEA MAZURI AMBAYO ANAYAFANYA RAIS SAMIA

Meza kuu ikiimba Wimbo mara baada ya Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana alipowasili kufungua Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM)

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) Ndg. Marry Chatanda akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Mbili kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana Akipokea tuzo ya pongezi kwa Kuchaguliwa kuendelea kuwa Makamu Mwenyekiti wa (CCM) Tanzania Bara kwa Mwenyekiti Ndg Marry Chatanda (Kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti Ndg. Zainab Shomari (Kulia) iliyotolewa katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM)

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana akifungua Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM)

Washiriki wa Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) ambao pia ni Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya wakiburudika na Nyimbo za Chama Cha Mapinduzi pamoja Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Zainab Shomari Akitoa neno la Shukrani mara baada ya Ufunguzi wa Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.

*************************


*WAELEZENI MAZURI YALIYOFANYWA NA RAIS Dk. SAMIA KUTEKELEZA ILANI YA CCM: KINANA*

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa CCM wayaeleze kwa wananchi mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kinana aliyasema hayo jijini hapa jana, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya.

“Katika maeneo yenu hakikisheni mnakisemea Chama na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia, wala msione haya kusema ili wananchi wajue na hata katika chaguzi zijazo tusipate shida.

Alisisitiza kuwa: "Chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia katika kipindi cha miaka miwili kila kata kuna alama ya maendeleo kuanzia shule, zahanati, barabara na maendeleo ya watu, tuna kila sababu ya kujisifia na kuusifia uongozi wa mwenyekiti wa chama hiki."

Vilevile, Kinana aliwataka viongozi wa UWT kubeba ajenda za wanawake kitaifa bila kuogopa jambo lolote.

KUHUSU UCHAGUZI

Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Kinana aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufia lengo la kujenga jamii yenye usawa.

Alisema mwakani kuna uchaguzi wa viongozi wa serikai za mitaa, hivyo ni vyema wanawake wakajitokeza kuchukua fomu kuomba nafasi mbalimbali za uongozi na CCM itawapa ushirikiano wa kutosha.

“Kuelekea uchaguzi ujao jiandaeni na kuwahimiza wanawake kuwania nafasi zote za uongozi na ninawahakikishia kuwa, CCM itawaunga mkono kwa hali na mali ili kuwa na wanawake wengi waliochaguliwa katika majimbo,”alisema.

ASISITIZA VIKAO

Katika hatua nyingine, Kinana aliwataka UWT kuhakikisha maamuzi mengi yanafanyika kupitia vikao na sio maamuzi ya mtu mmoja au kikundi cha watu.

Alisisitiza kuwa hata kiongozi anapokosea sio busara kumuamisha kituo cha kazi kabla ya kumuita na kumsikiliza kwani utakuwa ni ukiukwaji wa haki.

“Niwasihi tumieni vikao kuamua mambo sio kikundi cha watu, kila kitu lazima kijadiliwe kwa kina na kipite kwa hoja kwa sababu ndani ya CCM hakuna maamuzi ya mtu mmoja au amri, ninyi katika maeneo yenu hakikisheni ndani ya vikao huko ndio haki ya mtu itapatikana.

“Wenyeviti mpunguze kuhamisha watu hovyo, kama mtu amekosea aitwe aelezwe kosa sio kuchukua maamuzi ya haraka una muhalibia mtu mwelekeo, tujenge utamaduni wa kuambiana ukweli na msiogopane mtu anapokosea,”alisema.

Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM aliwashauri viongozi kusoma vitabu mbaimbali vya Chama ikiweo Ilani ya uchaguzi, sera, kanuni na katiba kwani vitawasaidia katika masuala mbalimbali ya uongozi.

Alisema CCM ni miongoni mwa vyama vichache duniani ambayo vinamaandishi mengi.

“Someni katiba, kanuni, ilani na sera kwani vitawasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za Chama na kuongoza kwa kuzingatia misingi ya haki,”alisema

UWT WAELEZA

Awali, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Marry Chatanda, alisema wanawake wanaridhika na kazi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia kwani ilani ya CCM inatekelezwa kwa kishindo.

Alisema katika kipindi cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita hakuna kilichosimama ndio maana waliandaa hafla ya kumpongeza Rais Dk.Samia kwa kazi nzuri alizozifanya.

“Sisi wanawake wa CCM hakika tumeridhishwa na uongozi wa Rais Dk.Samia na tunaahidi katika uchaguzi wa mwaka 2025 tutatoa fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu mwanamke mwenzetu,”alisema.

Kwa upande wake, Katibu wa UWT Taifa Dk. Philis Nyimbi alisema lengo la mafunzo hayo ni kuleta ustawi na kuwapatia viongozi maarifa namna ya kuongoza jumuiya hiyo katika ngazi zote.

Alisema mafunzo hayo yamewakutanisha viongozi 478 ambapo baada ya kumaliza elimu waliyoipata wataipeleka katika ngazi ya kata na matawi.

“Mafunzo haya ni mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wetu ukizingatia tunaelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2025, hivyo kutokana na mafunzo haya watatakiwa kuyapeleka katika ngazi ya kata na matawi na kutuletea taarifa,”alifafanua.

Post a Comment

0 Comments