Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS.DKT.HUSSEIN MWINYI AONGOZA MKUTANO WA JUKWAA LA KUMI NA MBILI LA BIASHARA ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa (SMIDA) Bw. Soud Said Ali, akitembelea maonesho ya Wafanyabiashara katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 19-3-2023, wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Kumi na Mbili la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Jijini Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Plastic Technology Enterprises Bw. Multala S.Juma, wakati akitembelea maonesho ya Wafanyabiashara Zanzibar, kabla ya kuongoza Mkutano wa Jukwaa la Kumi na Mbili la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B”Unguja leo 19-3-2023.(Picha na Ikulu)

WAJUMBE wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiongoza Mkutano wa Jukwaa la Kumi na Mbili la Biashara Zanzibar uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 19-3-2023 Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiongoza Mkutano wa Jukwaa la Kumi na Mbili la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 19-3-2023, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitoka katika ukumbi baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jukwaa la Kumi na Mbili la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana lililofanyika leo 19-3-2023.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments