Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NCHEMBA ATETA NA WAWEKEZAJI NCHINI UINGEREZA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Royal Africa Society, Dkt. Nicholas Westcott (kushoto) wakati wa Mkutano na jumuiya ya wafanyabiashara wa Uingereza jijini London. Mkutano huo ulilenga kuwashawishi wafanyabiashara hao kuwekeza nchini Tanzania, Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu-Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil na Balozi wa Tanzania-Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) akiagana na Mkurugenzi wa Shirika la Royal Africa Society, Dkt. Nicholas Westcott (Kulia) baada ya mazungumzo yao wakati wa Mkutano na jumuiya ya wafanyabiashara wa Uingereza uliolenga kuwashawishi kwa ajili ya kuwekeza nchini Tanzania, jijini London, Uingereza.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akihutubia katika Mkutano na jumuiya ya wafanyabiashara wa Uingereza wenye lengo la kuwashawishi kuwekeza nchini Tanzania, Mkutano huo umefanyika jijini London, Uingereza na ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu-Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil, na Balozi wa Tanzania-Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro, wakifuatilia matukio ya Mkutano kati ya Ujumbe wa Tanzania na baadhi ya Wawekezaji na wafanyabiashara Jijini London, Uingereza.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, London, Uingereza)

Post a Comment

0 Comments