Ticker

6/recent/ticker-posts

DC SAME AMSHUKURU RAIS DKT SAMIA KWA KUIWEZESHA HIFADHI YA TAIFA YA MKOMAZI KUONGEZA WATALII

MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lengo likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani.
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni kushoto akizungumza na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi wakati alipofika kwenye hifadhi hiyo kuitembelea ikiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani

Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Hifadhi hiyo na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu





Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi kulia akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni wakati wa ziara yake kwenye hifadhi hiyo

Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni katika akiwa ni Meneja wa Benki ya CRDB wilaya ya Same kulia

Watalii wakifurahia utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi

Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi

Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi

Tembo akiwa na mtoto wake katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi




Twiga akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi






Na Oscar Assenga aliyekuwa KILIMANJARO



MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amesema wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa ubunifu mkubwa alioufanya kupitia Filamu yake ya Royal Tour na matunda yake kuonekana kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kuhamasisha utaliiwa ndani ambapo alisema kwamba baada ya ziara hiyo watalii wanaoingia kwa mwaka sasa wameongezeka na kufikia zaidi ya 7000.

Alisema kwamba huo ni ubinifu wa kipekee ambao umefanywa na Mkuu huyo wa nchi katika kuhakikisha anatangaza vivutio vya utalii hapa nchini ikiwa ni kuhamasisha watanzania na w ageni kutoka nje kutembelea hifadhi zilizopo hapa nchini.

Mkuu huyo wa wilaya alisema pia Rais Dkt Samia Suluhu kupitia fedha za Tozo na Fedha za Covid 19 zimewasaidia kuimarisha miundombinu ya hifadhi nchini ambapo miongoni mwa hifadhi ambazo zimenufaika ni mkomazi ambapo kuna majengo ya utawala na barabara nzuri ambao zinahamasisha watalii hivyo Rais amekuwa mfano nzuri wa uhifadhi nchini.

Aidha pia alisema wanapokuwa na hifadhi inayofikika kirahisi wanapata watalii wengi ambazo wanasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu

Hata hivyo aliwahimiza watanzania kutembelea hifadhi za hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo kuwataka pia wananchi wa wilaya ya Same watumie wikiendi zao kuweza kufika mkomazi kuweza kuona vivutio vilivyopo na hivyo kusaidia serikali kuingiza mapato ambayo yatasaidia maendeleo kwenye wilaya yao.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na kupelekea fedha za Uviko ambapo waliweza kuzitumia kujenga lango maalumu ambalo ni la kuingilia wageni wanaofika kutembelea hifadhi hiyo na kuweza kupata huduma nzuri za utalii.

Alisema kwamba kupitia fedha hizo wameweza kujenga barabara nzuri yenye utefiu wa zaidia ya kilomita 140 na pia kutengeneza viwanja vya ndege na hiyo imetoa fursa kwa wageni ambao hawana muda wa kutembea kwenye magari kwa muda mrefu wakati wa safari zao kutoka maeneo mbalimbali kwenda kuitembelea hifadhi hiyo

Happiness alisema kwa kujengwa uwanja huo kumesaidia wageni kusafiri kutumia ndege kufika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi moja kwa moja kutoka kwenye viwanja vyengine

Post a Comment

0 Comments