Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE PIC YATEMBELEA MIRADI YA NHC JIJINI DAR ES SALAAM

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC, imeishauri Serikali kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi mbalimbali nchini katika kutekeleza miradi mbalimbali ili kuhakikisha miradi ambayo wanaisimamia iweze kuisha kwa wakati.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Jerry Silaa Wakati walipotembelea Miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC Jijini Dar es Salaam, ambapo wametembelea mradi wa Morocco Square, Mradi 7/11 uliopo kawe pamoja na Mradi wa Samia Housing Scheme uliopo tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es salaam.

Amesema Mashirika ya umma yameundwa kufanya kazi ya kutengeneza faida kwa kuhakikisha wanafanya mipango ili kufikia malengo waliojiwekea kama miradi ya Morroco square na 7/11 ambayo imegharimu Taifa.

"Shirika la nyumba NHC ni Shirika mkombozi kwa makazi ya mtanzania kwakuwa wamekuwa wakirahisha kwenye ujenzi wa nyumba ambapo unanunua nyumba ambayo imeshajengwa tayari na kuokoa muda wa kusimamia ujenzi" amesema Mhe.Jerry.
 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) Bw. Hamad Abdallah, ameishukuru kamati ya bunge hiyo kwakutenga muda wao na kuthamini majukumu ambayo wamepewa na taifa ya kusimamia mashirika ambayo yanafanya uwekezaji.

Amesema mradi wa Morocco Square umekamilika kwa asilimia 97 na muda si mrefu wataruhusu wapangaji, na Mradi wa Samia Housing Scheme unaendelea na ujenzi na wanatarijia kumaliza mwisho wa mwaka huu wenye nyumba takribani 560 na wanunuzi wameshapata kwa asilimia 80.

Aidha amemuhakikishia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC kusimamia miradi hiyo kwa gharama sahihi ikiwemo vifaa kuchukua moja kwa moja kutoka viwandani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC Mhe.Jerry Silaa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC Jijini Dar es Salaam, ambapo wametembelea mradi wa Morocco Square, Mradi 7/11 uliopo kawe pamoja na Mradi wa Samia Housing Scheme uliopo tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC aakitembelea Mradi wa Samia Housing Scheme uliopo tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es salaam. wakati wa ziara yao ya kutembelea Miradi ambayo inasimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Aprili 30,2023 Jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC akitembelea Mradi wa Morocco Square katika ziara yao ya kukagua miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Aprili 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Nyumba la Taifa ( NHC) Bw. Hamad Abdallah akieleza jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC mara baada ya kutembelea Mradi wa Morocco Square katika ziara yao ya kukagua miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Aprili 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Nyumba la Taifa ( NHC) Bw. Hamad Abdallah akieleza jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC mara baada ya kutembelea Mradi wa Morocco Square katika ziara yao ya kukagua miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Aprili 30,2023 Jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC wakiwa katika nyumba za Mradi wa Morocco Square katika ziara yao ya kukagua miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Aprili 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC wakiwa kwenye moja ya chumba katika Mradi wa Morocco Square katika ziara yao ya kukagua miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Aprili 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Nyumba la Taifa ( NHC) Bw. Hamad Abdallah akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC wakati wakiwa katika ziara yao ya kukagua miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Aprili 30,2023 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


Post a Comment

0 Comments