Ticker

6/recent/ticker-posts

KONGAMANO LA SAYANSI NA BUNIFU KUFANYIKA JUNI 14-16, 2023 JNICC

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), DkT. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za COSTECH leo Aprili 4,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), DkT. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za COSTECH leo Aprili 4,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), DkT. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za COSTECH leo Aprili 4,2023 Jijini Dar es Salaam.


***************************


Tume ya Sayansi na Teknolojia –COSTECH imeiomba Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kumualika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kushiriki kwenye Kongamano la Kongamano la Kitaifa na maonyesho ya Sayansi na Ubunifu linalotarajiwa kufanyika Juni 14-16 mwaka huu.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu wakati akizungumzia kuelekea kufanyika kwa Kongamano hilo ambalo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam


Dkt Nungu amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kuwawezesha watafiti,wabunifu na wanasayansi kukutana pamoja ili kujadili na kubadilishana mawazo na kupeana taarifa za masuala ya teknolojia na ubunifu nchini.


Aidha amesema kuwa Kongamano hilo ni mkakati wa Tume katika kutekeleza jukumu lake kwa kuwahabarisha watanzania kuhusiana na kazi zinazoendelea nchini na mashirikiano yaliyopo kwa watafiti wandani na nje ya nchi.


‘Katika malengo hayo tumenyumbulisha mambo mbalimbali ikiwemo kuishauri serikali na vyombo vyake kupitia matokeo ya kitafiti zinazofanywa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu lakini pia watafiti na wabunifu kupata fursa ya kusikiliza kutoka kwa wafanya maamuzi na watunga sera kuhusu mipango ambayo watafiti na wavumbuzi waweze kuifata miongozo hiyo’amesema Dkt Nungu


Dkt Nungu amesema kuwa kongamano hilo kutakuwa na mijadala mbalimbali sambamba na kuonyesha bunifu ambazo zimefanywa na wabunifu kutoka maeneo mbalimbali.


Dkt Nungu ameendelea COSTECH itaendelea kuwaunga mkono vijana wabunifu ili waweze kunufaika na bunifu mbalimbali wanazozifanya.

Post a Comment

0 Comments