
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar kushiriki dua ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Chama katika dua ya pamoja ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika kumbukizi ya miaka 51 ya kifo chake leo tarehe 07 Aprili 2023 iliofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika kumbukizi ya miaka 51 ya kifo chake leo tarehe 07 Aprili 2023 iliofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, viongozi mbalimbali pamoja na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakiomba dua mbele ya kaburi la Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika kumbukizi ya miaka 51 ya kifo chake leo tarehe 07 Aprili 2023 iliofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar.
0 Comments