Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZAZI WASIWARUHUSU WATOTO WAO KWENDA DISKO,VIBANDA UMIZA SIKU YA PASAKA.


Jeshi la polisi mkoani shinyanga limetoa tahadhari kwa wakazi woto wa mkoa wa shinyanga kuelakea sikukuu za pasaka Aprili 9, 2023 kuhakikisha wazazi wanakua na watoto wao, kutowaruhusu Watoto kwenda kwenye kumbi za starehe, disko na vibanda umiza.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoani shinyanga ACP Janeth Magomi amewataka watumiaji wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote za barabarani ili kuepuka ajali

Aidha kamanda Magomo amewahakikishia wakazi wote na washerehekeaji wa sikukuu ya pasaka kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuhakikisha washiriki wa sherehe hiyo wanakua salama, huku akiwatakia kheri ya sikukuu ya pasaka wakristo na wanashinyanga kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments