Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT.HUSSEIN MWINYI AANDAA FUTARI KWA WANANCHI MKOA WA KUSINI UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja jana mara baada ya Futari aliyowaandalia Wananchi wa Mkoa huo,iliyofanyika katika Ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Hall Tunguu. [Picha na Ikulu] 06/04/2023.
Wanawake katika shehia mbali mbali za Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi jana,katika katika Ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Hall Tunguu Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. [Picha na Ikulu] 06/04/2023.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (katikati) akitia chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi leo kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja, hafla hiyo imefanyika jana katika Ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Hall Tunguu Wilaya ya Kati. [Picha na Ikulu] 06/04/2023.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wan ne kulia) pamoja na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika swala ya Magharibi jana kabla ya Futari aliyowaandalia Wananchi wa Mkoa huo,iliyofanyika katika Ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Hall Tunguu. [Picha na Ikulu] 06/04/2023.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika Ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Hall Tunguu Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi jana. [Picha na Ikulu] 06/04/2023.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid (kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi (wa pili kushoto) jana baada ya Futari aliyowaandalia kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguija, katika Ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Hall Tunguu. [Picha na Ikulu] 06/04/2023.

Post a Comment

0 Comments