Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBACHAWENE AFANYA KIKAO KAZI NA WATENDAJI WA OFISI YAKE PAMOJA NA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YAKE ILI KUJIPANGA KIUTENDAJI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa na Naibu Waziri wake, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakijadiliana jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala bora, Bw. Xavier Daudi mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Mhe. Simbachawene na watendaji wa ofisi yake pamoja na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo kwa Kamishna wa Maadili, Mhe. Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bi. Neema Mwakalyelye mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Mhe. Simbachwene na watendaji wa ofisi yake pamoja na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Ndomba mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Boniface Simbachawene na watendaji wa ofisi yake pamoja na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo mara baada ya kikao kazi cha Waziri Simbachawene na watendaji wa ofisi yake pamoja na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa ofisi yake mara baada ya kikao kazi chake na watendaji wa ofisi hiyo pamoja na taasisi zilizo chini ya ofisi yake kilichofanyika leo jijini Dodoma. Wa pili kutoka kulia waliokaa ni Naibu Waziri wake, Mhe. Ridhiwani Kikwete, wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi, wa kwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala bora, Bw. Xavier na wa kwa kwanza kutoka kulia ni Kamishna wa Maadili, Mhe. Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi.

Post a Comment

0 Comments