Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUSIMAMIA HAKI NA KUTUNZA AMANI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023
Sehemu ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKT) Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza wakiwa katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipokea zawadi ya picha kwa niaba ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo wilayani Ilemema mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle akizumgumza katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwaongoza waumini katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera Askofu Dkt Benson Bagonza akizungumza mara baada ya kuchangia Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwamza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha saa iliyotolewa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa ajili ya kunadiwa ambapo saa hiyo ilinunuliwa kwa shilingi milioni 2.625 wakati wa Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na viongozi wengine wakitoka katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle akihitimisha Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ujenzi wa shule wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

******************


Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa amewataka viongozi wa dini nchini kuhakikisha wasimamia haki na kuienzi na kusimamia amani kwa manufaa ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.


"Niwasihi sana ninyi viongozi wetu wa dini kutukumbusha mara kwa mara sisi, waumini na watu wote kuhusu umuhimu wa kusimamia haki na kudumisha amani na kuiombea nchi yetu na viongozi wake" alisema Majaliwa.


Majaliwa alisema hayo leo tarehe 16 April 2023 katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Imani wilayani Ilemela mkoani Mwanza.


kupitia harambee hiyo ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria-Mwanza Kanisa hilo limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 119,563,000 zikiwemo fedha taslimu, ahadi na vifaa.


Kupitia hotuba yake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka viongozi wa dini nchini kutochoka kufundisha na kulea vijana katika maadili mema na kuthamini kufanya kazi halali.


" Katika nyakati hizi ni ukweli ulio wazi kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii yeru, vitendo viouvu na mambo yasiyopendeza mwenyezi Mungu yanazidi kuongezeka mambo ambayo siku za nyuma yalikuwa nadra sana kutokea au kusikia lakini sasa yanakuwa habari za kila siku na wakati mwingine huonekana eti ya kawaida" alisema majialiwa kupitia hotuba yake.


Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, kushuka kwa maadili ni jambo lenye athari mbaya kwa jamii na taifa kwa ujumla hivyo kunachangia sana na kurudisha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo na kuifanya kazi ya kuondoa umasikini kuwa ngumu.


Amesema, anaamini kwa dhati kuwa viongozi wa serikali, dini na vyama vya siasa wakishika mafundisho ya dini na kuwa na hofu ya mungu maovu mengi yatapungua na nchi kuoongozwa vizuri.


" Naendelea kuwaomba kwa niaba ya serikali, viongozi wa dini zetu zote tusaidiane kukea taifa letu kimaadili na tuweke mkazo zaidi kwa vijana kwa sababu kwanza wao ndiyo wahanga wakuu wa maovu yanayotendeka lakini pia wao ni taifa la leo na viongozi wa kesho" alisema


Kupitia hotuba yake hiyo, Majaliwa alisisitizia pia suala la elimu na kueleza kuwa elimu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote na kutaka viongozi wa dini kusaidia kuzungumza na wazazi na kuwaslimisha kuhusu umuhimu wa kusomesha watoto.


Amelipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria -Mwanza na waumini kwa ujumla kwa kujitoa kwa hali na mali kwa kufanya kazi ya Mungu kwa kuhakikisha jengo linakamilikia hasa ikizingatiwa fedha zote ni michango ya waumini na kubainisha kuwa, kitendo kilichofanyika ni chema na kinaleta baraka zote.


Awali Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle alisema ujenzi wa shule ya kanisa hilo unakadiriwa kuwa na gharama ya Shilingi 2,350,000,000 ambapo amesema mpaka sasa kiasi cha 430,000,000 kimetumika kujenga boma la madarasa kumi na boma la jingo la utawala.


Katika harambee hiyo ya ujenzi wa shule Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alichangia shilingi milioni 5 ili kutumika kukamilisha kazi ya ujenzi wa shule huku Dkt Mabula kuchangia milioni 2 katika ujenzi huo.

Post a Comment

0 Comments