Ticker

6/recent/ticker-posts

DC TEMEKE ATEMBELEA BANK YA AKIBA KATIKA TAMASHA LA KIJANA JANJARUKA.

Afisa masoko wa Benki ya Akiba Bw. Anthony Kunambi (mwenye fulana nyeusi) akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mwanahamisi Munkunda alipotembelea banda la benki hiyo katika viwanja vya Zakhem Mbagala kwenye tamasha la Kijana Janjaruka siku ya tarehe 22 Mei, 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Mwanahamisi Munkunda akizungumza na Afisa Masoko ya Akiba Banki Bw Anthony Kunambi akimweleza Mkuu wa Wilaya huyo fursa zinazopatikana katika benki hiyo wakati alipotembelea banda la Akiba Bank kwenye Tamasha la Vijana linalojulikana kwa "Kijana Janjaruka "


*********************

Na Mwandishi wetu

Akiba Commercial Bank Plc imekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya fedha kwa vijana na umma kwa ujumla hususan katika nyanja ya kujiwekea Akiba, huduma za Mikopo, mpango wa fedha na kupanga bajeti za mtumizi binafsi na Biashara ili kusaidia kukuza Uchimi wao.

Aliyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Munkunda wakati alipotembelea tamasha la vijana linalojulikaba kwa "Kijana Janjaruka " ambapo na Akiba Commercial Bank Plc ilishiriki kikamilifu lililoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambalo lilianza Mei 20-24 ,2023 katika viwanja vya Zakhem-Mbagala lengo la tamasha hilo ni kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana na maeneo ya jirani, kualika taasisi za fedha hususan mabenki ili kutoa elimu ya fedha kwa vijana na Akiba Bank kuonyesha bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na mabenki na taasisi nyingine.

Mkuu wa Wilaya Mwanahamisi alitembelea banda la Akiba Commercial Bank Plc katika viwanja hivyo siku ya tarehe 22 Mei, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kufahamu fursa mbalimbali zitolewazo kwa vijana kupitia Benki ya Akiba hususan huduma za Bima za BODASURE ambayo inalenga kutoa ulinzi kwa wamiliki na waendesha bodaboda na Bajaji.

Pia Mkuu Wilaya aliona fursa iliyozinduliwa na benki ya Akiba akaunti maalum kwa ajili ya Wanawake inayoitwa akaunti ya WARIDI ambayo ina masharti nafuu sana ya uendeshaji, lengo ni kuwainua Wanawake katika kufikia ndoto zao za mafanikio katika ujasiriamali.

"Mkuu wa Wilaya ya Temeke amefurahi na ameishukuru benki ya Akiba kwa kuonyesha mfano wa kuigwa kwa kutoa huduma bora jamii hivyo ameahidi kuendelea kushirikiana na taasisi za fedha hususan mabenki katika kuchochea maendeleo endelevu ndani ya Manispaa ya Temeke na Taifa kwa ujumla"amesema Mwanahamisi

Tamasha hilo lilifungwa siku ya tarehe 24 Mei, 2023 huku likikadiriwa kukusanya zaidi ya vijana laki 2 kutoka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Temeke walionufaika kupata elimu ya fedha

Post a Comment

0 Comments