Ticker

6/recent/ticker-posts

SILENT OCEAN YAFUNGUA OFISI MPYA NCHI INDIA -MUMBAI KUSAFIRISHA MIZIGO KUAZIA SIKU 17-25


NA Magrethy Katengu

SILENT OCEAN kampuni ya Usafirishaji imekuja na suluhisho la usafirishaji mizigo kutoka nchi India kwa muda kuanzia siku 17-25 ambapo hapo awali mizigo ilikuwa ikisarishwa hadi kufika Tanzania ilikuwa ikitumia miezi 3-6 hali iliyokuwa ikisababisha bidhaa nyingine kufika zikiwa zimepoteza ubora na kupelekea hasara . 

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Mohammed Soloka wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi Mpya iliyoanzishwa Mumbai nchini India amebainisha kuwa wamesogeza huduma bora kwa wafanyabiashara wanaotoa bidhaa zao nchini India na watawasafirishia kwa njia ya bahari na katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Marekani,China kwa muda mfupi . 

“Kampuni yetu ya Silent ocean iliona kwa mbali jinsi wafanyabishara adha waliyokuwa wanapata kwa kusafirisha mizigo kwa muda mrefu na bidhaa zao nyingine zilifika zikiwa zimepoteza ubora hivyo tuliona changamoto hiyo ya kuchelewesha kwa mizigo kufika nchini tukaamua kufungua ofisi hii,” amesema Soloka.




Mfanyabiashara wa bidhaa za Viatu Mitandio, nguo za kihindi Wahidi Abdul amesema hapo awali kabla ya Silent ocean walikuwa wanapata adha ya kusafirisha mizimo yao kwa gharama ya juu kwa njia ya ndege wakitaka ifike na ndege inachagua mizigo ya kusafirisha hivyo ufumbuzi umepatikana Sasa.

"Usafirishaji mizigo kwa njia ya ndege ni lazima ununue begi utalalofuatana nalo linagharimu dola za marekani milioni 80-50 hivyo inampa uzito mtu mmoja kubeba mabegi manne au matano hivyo kampuni hii imekuja na ufumbizi wa changamoto hii tuliyokuwa tunateseka kwa muda mrefu

Naye Sada Malkanza Mfanyabiashara wa Urembo, vitu vya Watoto, mitandio, amesema Sailent ocean ni Simba wa bahari ambapo ni muarobaini wa kusaidia Wafanyabishara bidhaa kwa muda mfupi kutoka Tanzania hadi India bila usumbufu.




Nae Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabishara Kariakoo, Abdalah Mwinyi wanahaki ya kuwashukuru Silent Ocean kutokana na kurahisisha na kufika kwa wakati mizigo ikilinganishwa na miaka ya nyuma ilikuwa ikisafirisha kwa njia ya meli miezi 3-6

"Siku hizi mbili tunapitia kwenye wakati mgumu tunaimani kikao cha kesho na Waziri Mkuu kitaleta matunda, tunashukuru Silent Ocean kwa kuongeza tawi lingine,".

Naye Mwakilishi wa Wafanyabishara, Wahid Abdulghafoor amesema wafanyabishara wa nchi hizi mbili walikuwa na changamoto ya usafirishaji wa mizigo hivyo kwa sasa wanahitaji kufanya kazi na Silent Ocean.

Post a Comment

0 Comments