Ticker

6/recent/ticker-posts

WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO TANGA WATOA HUDUMA ZA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI KWA WANANCHI

Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe akiwa kwenye eneo ambaalo huduma za upimaji kwa wananchi zinaendelea kwenye Hospitali hiyo ikiwa ni kuelekea siku ya maadhimisho ya Wauguzi Duniani
Wananchi wa Jiji la Tanga wakipatiwa huduma ya upimaji katikati Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe
Wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali
Wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali

Na Oscar Assenga Tanga

WAUGUZI katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo leo wameanza kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo utoaji wa Elimu ya Lishe Bora,utoaji wa chanjo ya Uviko 19,upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwa ni kuelekea siku ya maadhimisho ya sherehe ya wauguzi duniani inayo adhimishwa kesho Mei 5 mwaka huu.

Akizungumza leo Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe alisema kwamba watasherehekea siku ya wauguzi ambayo mwanzilishi wake Florence Nightingale; "Mwanamke wa Taa" ambaye alisimama kidete katika kuinua viwango vya uuguzi pamoja na kuwaelimisha Wauguzi kuwa na upendo kwa watu wenye uhitaji.

Tusiwe alisema kwa upande wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wao wataadhimisha siku hiyo kwa kutoa zawadi kwa wagonjwa na kuwafariji.

Tusiwe alisema kwamba pia watafanya upimaji wa sukari,Presha,VVU na Satarani ya Shingo ya Kizazi, shinikizo la damu ,huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kupima afya zao na kama kuna dalili za viashiria vyoyote aweze kupata huduma mapema.

Hata hivyo alitoa ushauri kwa wananchi ni muhimu wakajiwekea utaratibu mzuri wa kucheki afya zao mara kwa mara ili wanapogundulika na matatizo waanze kupata huduma za matibabu kwa haraka.

Post a Comment

0 Comments