Ticker

6/recent/ticker-posts

MABORESHO JESHI LA POLISI

Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ameweka wazi baadhi ya maeneo ambayo wizara imepanga kuyafanyia maboresho makubwa ili kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo.

Ameeleza adhma hiyo baada ya kumaliza kutoa maoni kwa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande huku vyombo vilivyopo chini ya wizara yake ni miongoni mwa taasisi ambazo tume hiyo inafanyia kazi pia katika uboreshaji huo,Tume hiyo iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo ikiwa kupitia taasisi na mifumo mbalimbali inayoshughulika na utoaji haki.

“Tunatimiza adhma ya Amiri Jeshi Mkuu,Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo ametaka kuona maboresho katika vyombo vya utoaji haki,hasa mambo yanayosababisha malalamiko kutoka kwa wananchi ambayo yamekua kero na yanaathiri haki za wananchi, kwahiyo maoni yangu niliyotoa yamelenga Zaidi kuleta mabadiliko ya kimuundo,kisheria na kikanuni na kuweza kuwa kuwa na vyombo vya polisi,magereza ambavyo havitakuwa na changamoto katika maeneo ya utendaji kazi .”alisema Waziri Masauni

“Maeneo ambayo nimetoa maoni na kama wizara tumedhamiria kuyaboresha ni eneo la Upelelezi,Ubambikizaji wa Kesi,Utoaji wa Dhamana na Mrundikano wa Mahabusu katika Vituo vya Polisi na Magereza, hayo yamekua maeneo ambayo tumekua tukipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.” Aliongeza Masauni

Katika kikao hicho waziri Masauni pia alipata wasaa pia wakubadilishana mawazo na wajumbe mbalimbali wa tume hiyo,wakiwemo Wakuu wa Jeshi la Polisi Wastaafu, Said Mwema na Balozi Ernest Mangu huku tume hiyo ikitarajiwa kukamilisha ukusanyaji wa maoni ifikapo mwezi April mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwasilisha maoni kuhusu mambo mbalimbali mbele ya wajumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai,tume hiyo imeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuangalia namna ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande.Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia),baada ya kikao cha kupokea maoni kutoka kwa waziri huyo kuhusu mambo mbalimbali. Tume hiyo imeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuangalia namna ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini.Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia),baada ya kikao cha kupokea maoni kutoka kwa waziri huyo kuhusu mambo mbalimbali. Tume hiyo imeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuangalia namna ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini.Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Post a Comment

0 Comments