Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM WAZINDUA KIGODA CHA UTAFITI WA KITAALUMA WA UHAMIAJI USIO WA HALALI

NA EMMANUEL MBATILO

CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kimezindua Kigoda Cha Utafiti wa Kitaaluma wa Uhamiaji usio wa halali ili kuangazia sababu za uhamiaji huo namna ya kuwahudumia na namna ya kuepuka uhamiaji usio halali.

Akizungumza katika Uzinduzi huo ambao umefanyika chuoni hapo leo Juni 1,2023 Jijini Dar es Salaam,Kaimu Makamu wa Chuo upande wa Taaluma Prof.Boniventure Rutinwa amesema utafiti utafanyika katika mazingira ya kawaida pamoja na kutoa elimu kwa watu kwa kutoa machapisho pamoja na kufanya semina mbalimbali.

Aidha amesema kuwa vita, uharibifu wa mazingira na miradi ya maendeleo ni kati ya vitu vinavyoweza kupelekea uhamiaji usio wa halali
Nae Msimamizi wa Utafiti Bi.Opportune Kweka amesema utafiti utahusisha washiriki 32 kutoka mataifa mbalimbali na vilevile utafiti huo unagusa utu wa wakimbizi hususan katika kupata kwao mahitaji muhimu.

Post a Comment

0 Comments