Ticker

6/recent/ticker-posts

Wananchi tunzeni vyanzo vya Maji fedha nyingi za serikali zinatumika katika miradi hiyo.


Na Shemsa Mussa, Kagera.

Wananchi wa Halmashauli ya Bukoba wametakiwa kutunza na kulinda vyanzo vya maji kutokulima na kukata miti karibu na vyanzo vya maji ikiwa miradi hiyo inatumia gharama kubwa za serikali .

Akiwa katika Mahojiano na Sayarinews Meneja Ruwasa Bukoba Eng Evaristo Mgaya,amesema kuwa kiasi cha shiling Milion 760 zilitengwa kwa ajili ya miradi wa maji uliyopo katika kata ya katoma utakaohudumia vijiji viwili vya kashenge na irango huku chanzo hicho kikikadiliwa kuwahudumia wanachi Elfu 7293.

Aidha amesema miradi ya maji kwa sasa wananchi wanatakiwa kulipia kiasi cha shiling 40 kwa ndoo kubwa yenye ujazi wa lita 20 huku wakilipia elfu 200 kwa unit 1 .

"Kila tiku katika uendeshaji wa maji ni ghalama Mlinzi, vifaa, watendaji wa kusimamia ,usafiri vyote hivyo ni ghalama hivyo mwananchi wachangia kiasi hicho tu kidogo ili zisiwepo lawama za kukwamishana, ameongeza Eng Mgaya".

Hata hivyo Eng Mgaya amesema mwaka jana mradi huo wa maji uliwekwa jiwe la msingi katika mbio za mwenge na mwaka huu unatarajiwa kuzinduliwa rasimi .

"Mradi umekamilika kwa asilimia zote na uilkuwa katika kipindi cha matazamio kwa muda wa miezi sita (6) na sasa upo kwenye miezi ya mwisho, amesema. Eng Mgaya .

Mwenge wa uhuru unatarajiwa kuanza mbio zake katika Halimashauri ya bukoba mnamo tarehe 10 Agost 2023.

Post a Comment

0 Comments