Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATEMBELEA BANDA LA COSTECH KWENYE MAONESHO YA KIMATAIFA YA WAKULIMA NANE NANE JIJINI MBEYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu kuhusu Tume hiyo inavyowasaidia wakulima wenye ubunifu mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika viwanja vya John Mwakangale kwa ajili ya kushiriki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane Kitaifa Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu kuhusu namna ya kuwapa chanjo Samaki wakiwa ndani ya maji katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwanzilishi wa Kampuni ya Avomeru Bw. Jesse Oljange kuhusu ukamuaji wa mafuta mbalimbali ikiwemo ya zao la parachichi katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

Post a Comment

0 Comments